Home Search Countries Albums

Mnachangaya

NACHA

Mnachangaya Lyrics


yasubi ndani ya mbanyu
 
Habari ndugu zangu marafiki jamaah
Nimesimama hapa kuwakilisha mtaa
Kwa usahihi na ufasaha mimi naitwa Nacha
Almaarufu Sandi Manara naamini mnanipata
 
Taarifa njema kwamba nimealikwa na mzee
Mimi na yeye meza moja tuongee
Okey, usilete mambo ya uoga
Mtaani ni kugumu, kutwa tunakula zoga
 
Mmmh, kugumu kivipi? Kutwa mnabeti
Instagramu peji zenu, picha za uchi mnaposti
Wasanii kufungiwa kucha kutwa yaani nuksi
Tatizo wasanii na nyinyi daily matusi
 
Madada wanaojiuza huku danguroni
Ah-ah, mimi siwezi kuongea na mzee mambo ya kihuni
Madawa hospitali, eeh hilo nitamwambia
Viwanda alivyosema, hilo nitamwambia pia
Wabunge kutukana bungeni bila siri
Siwezi kusema kuna kamati ya maadili
Hmmh, jeti neki hio ndo balaa
Mi siwezi nikasema, nyie mnataka nihame Dar

Aaah, eeh mbona mnachanganya
Unatoka wapi urafiki wa paka panya
Aaaah, ah kumbe tunaelewana
Kakwambia nani undugu ni kufanana

Aaaah, mbona mnachanganya
Unatoka wapi urafiki wa paka panya
Aaaah, kumbe mnaelewana
Kakwambia nani undugu ni kufanana

Naam, madawa yanaharibu wanamziki
Hamsaidie mtoto ila anayaahidi
Ashasaidiwa na bado hashikiki
Nimeamini kweli kunguru hafungiki

Mi nilitegemea labda mtakuwa na hamu
Kwanini Bongo kichwa cha mwendawazimu
Hamna kazi na mmesoma mpaka chuo
Vikasa vipo wapi kama elimu ni ufunguo

Tajwa mboga mboga, ushuru kwenye koo
Uswazi mvua zikinyesha wanazibua vyoo
Ah, ihalalishwe bangi, acheni akili za kizembe
Hivi mnajua, ya kuwa, shujaa jing'ua
Zina madhara kwenu, tena sanaa
Mwisho ya yote nitapiga naye selfie
Nikaposti Insta kwangu na peji ni private

Okey, nadhani tumeelewana
Kila mmoja wetu ana majukumu ya kufanya
Utawasilisha vile vyote vyenye maana
Ushindi wetu ni umoja pamoja waungwana

Aaah, eeh mbona mnachanganya
Unatoka wapi urafiki wa paka panya
Aaaah, ah kumbe tunaelewana
Kakwambia nani undugu ni kufanana

Aaaah, mbona mnachanganya
Unatoka wapi urafiki wa paka panya
Aaaah, kumbe mnaelewana
Kakwambia nani undugu ni kufanana

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2019


Album : Mnachangaya (Single)


Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

NACHA

Tanzania

Nacha Ousam is a musician from Tanzania. ...

YOU MAY ALSO LIKE