Home Search Countries Albums

Weupe Lyrics


Yeeeeh   hehee
Ooouuyeeeh  (toooooouuuch )
Baba ako

Hii dunia ukitumia wakati wako vizuri lazma mambo itajipa
Naongea na sad generation yenye happy pictures
Ukijiona zaidi fanya ya zaidi kwa uhakika
Ili usidate hata  kama wowowo haijakulipa
Sawa unaweza ukasonga bila fm walla stereo
Ila uwe  na juhudi , mungu  na kutumia akili  yooh
Ni kuchapa kazi kwa maadili ,  you pay mabill bro
Siwezi  kuwa sinza star tu na kuna  the bigg world
Msione nimetulia mkafikiri mi ni kiande
Mnataka kuharibu shughuli , kisa mmeona  mambo pambe
Hii ni keki ya taifa kila mtu ana kipande
Kwenye shamba la upendo mwana chuki usizipande
Leo nataka niongee fact nyie viziwi mnisikie
Marapper wanariadha  ulingoni  msikimbie
Waumini wangu kilinge leo naomba msiingilie
Hii sio show ya bure kama haulipi usiingie
Kwa mfano hiyo beef ya weusi na weupe i don’t like
Aliye kuinspire ni baba akikupiga don’t fight
Ku beef nae haiwezi kukufungua if yo tight

Utapoteza tu mida na chuki ndo ita ku bite
Wakati nyie mna hate wenzio wanavuka ma border
Mnageuka misukule na hakuna aliyewaloga
Na kama  unaleta  ubishi na wakati hauna hoja
Utabaki unajiita  uno na hauwezi kuwa namba moja
Ufalme wa rymes unaanzia kwenye nidhamu
Haustahili kama hauheshimu wengine wanachokifanya
Wengi kwa game  prof   ndo alitufanya tu come
Ningekuwa mtoa tuzo,  hizo time jay angezikusanya
Kwanza kikosi kazi hakina kazi za kufanya
Hamjifunzi kwa wakazi , mziki sio tu kuchana
Mna shida na interview na media mnazitukana
Nyimbo hatupigi show hatuwapi na hamna cha kutufanya
Mkimdiss  joh kisingizio eti marapa aliwanyea  
Mkamsifia ngwea  na alikuwa diss rapper is not fair
Mnafanya  tuone bendera ya hate inapepea
Wao wataacha legacy nyie mnaweza msiache hata fea
Alikuwa kwa industry toka mdogo  hadi anazeeka
Ukiona bado anabebwa ujue huyo mtu anabebeka
Nyie mmekuja kitambo hadi saa hii mnahenyeka
Na systerm iliwaelewa ila nyie  hamjaeleweka

Kuchukia ma legend wa game hii
Ni kama unachukia hilo darasa la cmg
Na wakati kila wakitoa hit ni omg
Embu msichanganye double kick kwa mo eti
Levo zenu hata sio mimi  labda lunya
Mngetudiss sisi marapa wenye kasi kama duma
Kumchokoza simba mzee ambaye hajachoka kutafuna
Ni kama kupiga sarakasi wakati unakunya
Uchawi ni kuamini huwezi  fika bila mtu
Unamwabudu mungu gani kwani ?? Ama mungu mtu ?
Lord ako na eyes ya kutuona  kila kona
Ndo maana alimleta g na  wanako tukapona

Mpaka najiuliza viko wapi vitendo dhidi ya kubonga
Mbona mitaa iko na njaa ya muziki zaidi ya kuponda
Ingekuwa ni mimi nigeacha kujiita songa
Na  kila siku niko pale pale kama mlima kitonga
Hamuwezi kuwa na ladha hata mtiwe chachandu
Nikiangalia dira mlipoteza tangu na tangu
Mna majengo makali ila yamezungukwa tandu
Mi sifanyi ngoma na jux halafu niimbie maisha yangu
Wote  lengo si ni kuwa kama rostam wa azizi
Sa kwanini mnatukana  rostam ya machizi
Wenzenu wako majuu nyie mko mtaani tu mnasizi
Wivu unawageuza wachawi ila hamna  tu hirizi
Ujue mi nawaangalia halafu siwapatii picha
Game mmefakisha mnajikuta maticha
Wakati wenu kwisha, mmebaki machicha
Hamna la kuimba hata nikiwapatia features
Joh  hawezi shuka  eti kwa kupondwa na azma
Mtu ambaye anaforce miaka kumi kutoka kwa lazma
Crew yenu mnafanana style kama mchele wa basmat
Ushafeli weka nguvu sasa kuikuza aznas

Kumaintain game si waliweza wengi tuu
Ay, fa , fid q , ama mr blue
Ila mwamba ndo mnaona wa kumfanyia maandamano
Au roho zinawauma kisa sisi sio wazaramo  
Hamuwezi kutoboa kwa hii stant
Ma sean p wa bongo na hamuafford kwa p funky
Kwa vile mmeleta   mawenge  tena   kwa hii chance
Na sisi hatuwezi kuwapa  uboy kwa hii country
Again

Weupeee, eeh
Weupeee, eeh
Si hatudeal na weupe  eeh
Toka zamani, wakali wafani
Na  ndo kinafanya waweuke eeh
Hatutaki utani tumetumwa money  
Si hatudeal na weupe  eeh
Toka zamani, wakali wafani
Na  ndo kinafanya waweuke eeh
Hatutaki utani tumetumwa money  
Yeeii yeeh

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2021


Album : Weupe (Single)


Added By : Farida

SEE ALSO

AUTHOR

MOTRA THE FUTURE

Tanzania

Motra The Future is a rapper from Tanzania. ...

YOU MAY ALSO LIKE