Home Search Countries Albums

Mwanangu Lyrics


CS Records
Mwanangu usikubali
Wenye dhambi wakushawishi
Mwanangu usikubali
Wenye dhambi wakushawishi

Mwanangu usikubali (usikubali..)
Wenye dhambi wakushawishi (Mwanangu eeh..)
Mwanangu usikubali (usikubali..)
Wenye dhambi wakushawishi

Wakisema njoo pamoja nasi
Na tuvizie ili kumwaga damu
Tumwotee asiye na haki eeh
Mwanangu usikubali
Wanamaneno matamu kama asali
Lakini mwisho mchumbu kama shubiri
Mwanangu usikubali
Wenye dhambi wakushawishi

[CHORUS]
Mwanangu usikubali (usikubali..)
Wenye dhambi wakushawishi (Mwanangu eeh..)
Mwanangu usikubali (usikubali..)
Wenye dhambi wakushawishi

Mwanangu usiende njiani pamoja nao
Usienende katika mapito yao
Mwanangu usikubali
Wenye dhambi wakushawishi
Miguu yao huenda mbio maovuni
Na hufanya haraka kumwaga damu
Mwanangu usikubali
Wenye dhambi wakushawishi

[CHORUS]
Mwanangu usikubali (mwanangu eeh..)
Wenye dhambi wakushawishi (Mwanangu ooh..)
Mwanangu usikubali (mwanangu eeh..)
Wenye dhambi wakushawishi

Mwanangu kumcha bwana ni chanzo cha maarifa
Bali wapumbavu hudharau hekima
Mwanangu usikubali
Wenye dhambi wakushawishi
Yasikilize mafundisho ya baba yako
Wala usiache sheria ya mama yako
Mwanangu usikubali
Wenye dhambi wakushawishi

Mwanangu mtego hutegwa bure ee
Mbele ya macho ya ndege yeyote
Mwanangu usikubali
Wenye dhambi wakushawishi
Lishike sana neno la mungu
Uli andike kwenye kibao cha moyo
Mwanangu usikubali
Wenye dhambi wakushawishi

[CHORUS]
Mwanangu usikubali (mwanangu eeh..)
Wenye dhambi wakushawishi (Mwanangu ooh..)
Mwanangu usikubali (mwanangu usiki eeh..)
Wenye dhambi wakushawishi

Uwe jasiri kama simba
Mpole ee kama njiwa
Mwanangu usikubali
Wenye dhambi wakushawishi
Mshike sana elimu
Usimwache aende zake
Mwanangu usikubali
Wenye dhambi wakushawishi
Heshimu wakubwa kwa wadogo
Tajiri na fukara
Mwanangu usikubali
Wenye dhambi wakushawishi

 [CHORUS]
Mwanangu usikubali (mwanangu..)
Wenye dhambi wakushawishi (Mwanangu eeh..)
Mwanangu usikubali (mwanangu ooh..)
Wenye dhambi wakushawishi

Mwanangu usikubali
Wenye dhambi wakushawishi
(yeeyeeyee) usikubali
Wenye dhambi wakushawishi

 

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2018


Album : Mwanangu (Single)


Added By : Afrika Lyrics

SEE ALSO

AUTHOR

CHRISTINA SHUSHO

Tanzania

Christina Shusho is a Gospel  artist from Tanzania. ...

YOU MAY ALSO LIKE