Kijuso Lyrics

Unaringa kitu gani we mwenyewe ujisute
Afadhali hata Nyani sio we Mwanamke
Hupendezi asilani so unyoe au usuke
Nilifuata kitu gani umefanya nijute
Hah
Mimi nakonda pungua eeeh na usikurupuke
Kwanza naongea na nani naomba nikumbushe
Mimi na wewe hatuendani jipandishe jishushe
Usinipande kichwani namba yangu ifute
Hizo dharau mwanamke ulopata
Naona unasahau nyuzi zako nilikata
Nimepanda dau mkataba nimekata
Tena Nyang'au ndo ukome kunifuata
Unaringa una nini kijuso
Vijimeno kama Jini Gaucho
Kwani nawe una nini Kituko
Uso na kazi mjini Upo upo
Punguza kelele mama acha kelele mama kelele
Punguza kelele baba kelele acha kelele bwana kelele
Eti nawe unavimba perfume tu mtihani
Kwanza shati ulovaa umeazima kwa nani
Wanifuataa Kapuku utanipa nini
Nilikuachaa leo kimekuwasha nini
Funga bakuli mbele yangu wewe mshamba
Nakujua vizuri toka unavaa mabwanga
Wakati unanuka moshi huna hata ishu
Kwenye pochi wanja na tishu
Unapenda ganda la ndizi kuteleza
Wakati kupambana mpaka mchuzi wa Pweza
Dume zima tantalantala instagram inahu
Wakati kwenu kula kulala huchangii hata kitunguu
Hizo dharau mwanamke ulopata
Naona unasahau nyuzi zako nilikata
Nimepanda dau mkataba nimekata
Tena Nyang'au ndo ukome kunifuata
Unaringa una nini kijuso
Vijimeno kama Jini Gaucho
Kwani nawe una nini Kituko
Uso na kazi mjini Upo upo
Punguza kelele ooh kelele acha kelele mama kelele
Punguza kelele baba kelele acha kelele bwana kelele
Unaringa una nini kijuso
Sijui meno kama Jini Gaucho
Kwani nawe una nini Kituko
Uso na kazi mjini Upo upo
Punguza kelele mama kelele acha kelele mama kelele
Punguza kelele baba kelele acha kelele bwana kelele
WATCH VIDEO
ABOUT THIS SONG
Release Year : 2017
Album : Kijuso (Single)
Copyright : ©2017
Added By : Trendy Sushi
SEE ALSO
AUTHOR
RAYVANNY
Tanzania
Raymond Shaban Mwakyusa (born 22 August 1993), better known by his stage name Rayvanny, is a Tanzani ...
YOU MAY ALSO LIKE