Home Search Countries Albums

Mungu Yuko Bize

BWANA MISOSI Feat. CHEGE

Mungu Yuko Bize Lyrics


Aliumba mbingu nchi na bahari
Aliumba samaki pori wanyama wakali
Milima nyota mwezi mchana na juakali
Apewe sifa utukufu wala sikitendawili
Alimuumba dume adamu fahari
Akamuumba jike pia eva wake mwali
Akaleta ndoa ili waoane
Akasema kazi imebaki sasa mzaane
Hii hadithi ya kweli ya jana kama ya kesho
Alizaliwa abeli kaini musa na petro
Binadam unajifanya kwamba uko bize
Bize kuliko mungu alieumba bize
Aliumba mchana nabado akaleta mkesha
Akashuhudia vita akazikomesha
Ukamuomba akuponye na ukapona presha
Ukatengeneza gari leo unaliendesha
Mungu wa wamasai mungu wa mang’ati
Aliemfanya daudi mshinde goriati
Alimuumba na osama binladen miaka ya kati
Akamfanya huyu bwana asomee juu ya dawati
Anafanya dunia nzima iwe na umoja
Ili isiwe kama septemba kumi ma moja
Hana mfano kumsujudu kumuabudu kumtukuza
Peke ake kwamba yeye ndio muweza
Mengi amefanya nab ado miaka imekatika
Hajasema sasa basi minapumzika
Kaenda Kenya na Zimbabwe kwa samba wa nyika
Mugabe shangirai kibaki odinga washirika
Alimuumba rushahu akamzaa joseph
Akamuumba shabani akamzaa sefu
Aliuumba msamaha na akasamehe wakosefu
Nikipi unachofanya matendo masafi au machafu

Kila kitu unachofanya (unachofanya)
Mungu yuko bize zaidi yako
Kila kitu unachofanya (unachofanya)
Mungu yuko bize zaidi yako
Bizeee eeeeehh
Mungu yuko bize zaidi yako
Bizeee eeeeehh
Mungu yuko bize zaidi yako

Hii ni bize ya mungu ndugu isome kwa vina
Ubavu kibao kampa braza johnsiner
Kawapa vipaji ndugu venas na serena
Kawapa macho madogo wajapan na wachina
Kamuumba bruce lee akafa na jina
Kamuumba fagason kwa wale wapenzi wamanchesta
Kamuumba gaucho chuji bonan na ngasa
Kafanya taifa star kwasasa inakubalika
Kafanya bongo uchaguzi uwe na amani
Kamuweka zitokabwe katiba ramani
Kampa kikwete uenyekiti wa afrika
Kaipa nyumbani kigoma ziwa Tanganyika
Kafanya Obama ameika anakubarika
Huyu mungu wa ajabu mwenye kutawala naimba
Hajawahi kusinzia hajawahi kulala
Yuko bize zaidi ya bizebize kila idara
Kuna walemavu wazima wanamuonba yeye
Pia majambazi wachamungu wanamuomba yeye
Baraka za wote zitoke kwake yeye
Nani yuko bize nauliza zaidi ya yeye
Kuna wakristo huku kuna waislam
Kuna wachungaji huku kuna mahimamu
Bado kuna pepo huku jehanamu
Umekosa leo labda tomorrow ndio yako zamu
Kamuongoza zuma south afrika amekubalika
Kawapa naijeria psuare na 2face
Braza chacha na ditopile wamekufa na tetesi
Lakini kwa mungu yote hayo bado mepesi
Kanyongwa mtu maarufu sadam ameshuhudia
Yameundwa mabom kibao tu ya n’yukilia
Bado mungu anaisimamia
Kazi yake kubwa kuiponya hii dunia

Kila kitu unachofanya (unachofanya)
Mungu yuko bize zaidi yako
Kila kitu unachofanya (unachofanya)
Mungu yuko bize zaidi yako
Bizeee eeeeehh
Mungu yuko bize zaidi yako
Bizeee eeeeehh
Mungu yuko bize zaidi yako
Kila kitu unachofanya (unachofanya)
Mungu yuko bize zaidi yako
Kila kitu unachofanya (unachofanya)
Mungu yuko bize zaidi yako
Bizeee eeeeehh
Mungu yuko bize zaidi yako
Bizeee eeeeehh
Mungu yuko bize zaidi yako

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2022


Album : Mungu Yuko Bize (Single)


Added By : Farida

SEE ALSO

AUTHOR

BWANA MISOSI

Tanzania

Bwana Misosi is a musician from Tanzania. ...

YOU MAY ALSO LIKE