Home Search Countries Albums

Msukule

Y PRINCE Feat. FOUNDER TZ

Msukule Lyrics


Mmmh mmmh
Call me founder tz

Mbona sijafa nipo hai mnataka kunizikia aah
Mipango ya kusafirisha wengine wanasema tuzike hapa hapa
Mamaa ndo hunioni wala hunusikii mwanaoo
Msifanye mazishi nikiwa hai yatatimia malengo yaooo
Sio kifo cha ghafla wala ajali mungu msimlaumu bure
Munazika mgomba mi nipo hai wamenifanya msukule
Na kwenye msiba ndo wanalialia kama wema kumbe wabaya
Na kumbe wao ndo wamenichukua kunikata ulimi miksa midawa
Oouuuh oouuuuhh

Msukule
Kwahiyo hata shule sitosoma tena
Msukule
Hata familia yangu sitoiona daima
Msukule
Eeh mola wangu niteteee aah
Msukule

Karibu kwenye chama huku hakuna baba wala mama
Huku ni mwendo wa kazi kama si kufyeka ni kulimaa
Kuna muda nakuwa kiti kwenye vikao vyao
Nakuwa jembe kwenyemashamba yao
Ni mikikimikiki fimbo miksa vibao
Hata hiko chakula mpaka washibe waoo
Hakuna muda wa kupumzika kazi usiku na mchana
Matumaini nimeyashika nasubiri kudura za maulanaaa

Msukule
Ukiishiwa nguvu wanakukula nyama
Msukule
Huku ni kujikaza hakuna yelele mama
Msukule
Oooh loloh oooh
Msukule

Aaeeh aaeeh walimwengu wabaya
Aaeeh aaeeh tutakutana kwa mola
Aaeeh aaeeh walimwengu wabaya
Aaeeh aaeeh tutakutana kwa mola

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2023


Album : Msukule (Single)


Added By : Farida

SEE ALSO

AUTHOR

Y PRINCE

Tanzania

Y PRINCE is a young artiste from Tanzania. ...

YOU MAY ALSO LIKE