Chozi Lyrics
Kwetu kitanda cha kamba
Si godoro si shuka ni mkeka
Kibanda chenyewe chavuja
Aaah
Nyumba yenyewe ya kupanga
Shule nako majanga
Shati viraka
Viraka
Nikiangalia haya wazazi wangu
Namwonea huruma baba
Fundi mwenza, mbeba ngeze
Usawa umemkaba
Inamuuma roho mama yangu
Mwanawe anadhalilika
Shule ni ada, mida bwada
Nguo zimeraruka
Mama pressure inapanda
Dada naye mgonjwa sana
Kaka naye kapagawa
Yuko milembe
Baba sukari imebamba
Ndugu hawana msaada
Sote tuko njia panda
Yaani mawenge
Mang'amu ng'amu
Nadondosha chozi nakufuru Mungu
Mang'amu ng'amu
Shida kwangu ndo kimbilio
Mang'amu ng'amu
Hivi lini mimi nitapata nafuu
Mang'amu ng'amu
Oooh
Mtaani naitwa Kayumba
Mara muuza karanga
Mara muokota machupa
Aaah
Kila duka deni hatujalipa
Vikoba nao watutafuta
Yaani mchaka mchaka
Ninawaza sana
Lini tutapata na sisi?
Ututoke umasikini
Inamuuma roho mama yangu
Mwanawe anadhalilika
Shule ni ada, mida bwada
Nguo zimeraruka
Mama pressure inapanda
Dada naye mgonjwa sana
Kaka naye kapagawa
Yuko milembe
Baba sukari imebamba
Ndugu hawana msaada
Sote tuko njia panda
Yaani mawenge
Mang'amu ng'amu
Nadondosha chozi nakufuru Mungu
Mang'amu ng'amu
Shida kwangu ndo kimbilio
Mang'amu ng'amu
Hivi lini mimi nitapata nafuu
Mang'amu ng'amu
Oooh
WATCH VIDEO
ABOUT THIS SONG
Release Year : 2019
Album : Chozi (Single)
Copyright : (c) 2019
Added By : Huntyr Kelx
SEE ALSO
AUTHOR
YOU MAY ALSO LIKE