Mkono wa Bwana Lyrics
Mengi mazuri tumeyaona
Mungu umetenda
Ni kweli we muweza
Ulitamka vitu vikawa
Neno tu latosha
Ukisema umetenda
Bahari shamu Isiraeli
Ah uliwavusha
Kawatoa utumwani
Watumishi wako umewapa
Yote waombayo
Ikiwa umependezwa
Uamulo hakuna wa kulipinga
Hakika we ni Mungu wa vyote
Unatawala dunia na vilivyomo
Makuu umeyatenda Jehova
Tumeuna mkono wako Bwana
Matendo yako Bwana ni makuu mno
Umetutoa mbali
Ukatushika mkono
Mahali uliona pekee hatuwezi
Chini hata juu
Watu unawainua
Sifa na utukufu ni zako milele
Twasifu jina lako
Milele tutakusifu
Daima we umwema tutaishi kwako
Ona
Msalabani ulitufia
Hm ulitupenda
Dhambi zetu ukabeba
Baraka zako tuliziomba kweli tumeona
Hakika unabariki
Hata vipaji we ndo hutoa
Umetuwezesha
Tunaimba na kusifu
Walio haki hutowaacha
Uliwaahidi
Hata mwisho wa dahari
Hm watu wako umewapa mamlaka
Kwa jina lako Yesu
Waponye
Na huna ubaguzi
WATCH VIDEO
ABOUT THIS SONG
Release Year : 2016
Album : Mkono Wa Bwana
Copyright : ©2016
Added By : Trendy Sushi
SEE ALSO
AUTHOR
YOU MAY ALSO LIKE