Home Search Countries Albums

Nikubali Yesu

NEEMA GOSPEL CHOIR

Read en Translation

Nikubali Yesu Lyrics


Kuna vijito vya maji ya uzima
Mlimani mwa Bwana
Kila aogaye humo yuna usalama
Kila aogaye humo yuna usalama
Kama ungelijua karama yake Mungu leo hii
Ya kwamba ye ni nani aongeaye na wewe leo hii
Ungelimwomba Yesu akupe maji ya uzima tele
Ungelimwomba Yesu akupe maji ya uzima tele
Wala hakuna haja ya kusubiri maji yatibuliwe
Tena hakuna haja ya kusubiri mtu akuwezeshe
Ungelimwomba Yesu akupe maji ya uzima tele
Ungelimwomba Yesu akupe maji ya uzima tele

Kuna vijito vya maji ya uzima
Mlimani mwa Bwana
Kila aogaye humo yuna usalama
Kila aogaye humo yuna usalama

Je shida yako ni ipi?
Mwambie Yesu anaweza
Mwambie Yesu usinipite
Niko hapa Bwana
Nimejaribu mwenyewe pekeyangu nimeshindwa unisaidie
Yesu wewe unaweza
Yesu wewe unatosha
Yesu wewe usinipite
Usinipite Bwana
Nakuita Yesu
Nakuita Bwana
Nakuita

Sikia kuomba kwangu ee Yesu
Amani yangu ni wewe mfalme
Nimesikia habari zako,
nakimbilia kwako Bwana
Nisaidie, nisaidie
Nikubalie ombi langu Bwana nikuombalo
Usiniache peke yangu Bwana mimi sitaweza

Nikubalie ombi langu Bwana nikuombalo
Usiniache peke yangu Bwana mimi sitaweza
Nikubalie ombi langu Bwana nikuombalo
Usiniache peke yangu Bwana mimi sitaweza
Nikubali, nikubali
Ewe Yesu Bwana wangu
Ewe Yesu
Nikubali, nikubali
Ewe Yesu Bwana wangu
Ewe Yesu
Nikubali, nikubali
Ewe Yesu Bwana wangu
Ewe Yesu

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2020


Album : Nikubali Yesu (Single)


Added By : Farida

SEE ALSO

AUTHOR

NEEMA GOSPEL CHOIR

Tanzania

Neema Gospel Choir is a group of born again Christian Singers, members of Africa Inland Church (AICT ...

YOU MAY ALSO LIKE