Home Search Countries Albums

Mama Lyrics


Niko fresh niko poa
Asante Mungu kwa pumzi nayopumua
Nakuombea mama umenileta kwenye dunia
Leo utafurahi kidogo mi nawe tukiongea
Kwanza pole kwa msiba baba ametangulia
Najua una kazi nzito ya kuongoza familia
Kabla baba kufariki kuna mambo yalitokea
Wapo waliopenda wengine walichukia
Mama huenda baba anajua ni ukoo moja
Ila mama we na baba najua si kitu kimoja

Umejaliwa hekima busara na upendo
Inshallah tutafika mbali usipo badili mwenendo
Kuna baba wadogo hawa kuwa nao makini
Bado hawaamini kama ndo umeshika mpini
Waongo wanafiki wamejawa ufitini 
Wanaongoja uteleze ili wakupige chini

Hey mama we love you mama
Hey mama tunakupenda sana
Hey mama we love you mama
Hey mama tunakupenda sana

Tukificha maradhi kifo kitatuumbua
Mama  tusipoziba ufa hakika tutajenga ukuta
Kuna mambo ya msingi ni lazima kuyaongea
Mama sio kwa ubaya ni kujenga familia

Baba alikuwa mkali mama mwenyewe unajua
Yaani tuliishi kwa taabu japo kuwa ni wa kishua
Sio sisi tu mpaka wageni walikimbia
Kuhusu kaka yangu Ibra natumai ulisikia

Naye alikimbia ameacha mke na watoto pia
Wengine walipotea tu hatujua wako wapi?
Sema neno kuhusu hili mama ututoe wasiwasi
Mama njaa ikiuma tunaruhusiwa kusema
Ukikosea tunaruhusiwa kuongea
Au ndio kama baba mtu mzima hakosei?
Nina zawadi yako siku yako ya birthday

Hey mama we love you mama
Hey mama tunakupenda sana
Hey mama we love you mama
Hey mama tunakupenda sana

Mama hili la mwisho
Najua unajua kwamba, ukishatengea na familia yako
Huruhusiwi na unapoteza sifa za kushiriki kwenye vikao
Vya maendeleo ya ukoo

Lakini shangazi Halima na wenzake
Mbona bado nawaona kwenye vikao vya ukoo?
Na walishatengwa na familia yao?
Sema kitu kuhusu hili mama

All the best mama
Wajukuu zako nyumbani wanasubiri 
Nirudi na chochote kitu
Acha nikatafute

Hey mama we love you mama
Hey mama tunakupenda sana
Hey mama we love you mama
Hey mama tunakupenda sana

 

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2021


Album : Mama (Single)


Copyright : (c) 2021


Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

NAY WA MITEGO

Tanzania

Emmanuel Elibariki, popularly known as Nay Wa Mitego, or simply  Mr Nay,  is a Tanzanian r ...

YOU MAY ALSO LIKE