Home Search Countries Albums

Amkeni Lyrics


Nitakacho kiongea
Mnaweza niona sio mzalendo; zalendo zalendo gani
Inaendeshwa kimagendo
Wengine mwisho wa wimbo huu
Mtasema mi mchochezi
Kilakitu kiko wazi mama yenu analea wezi
Ndiyo anafuga wezi, hapa kikubwa dua
Hata report ya gag hakuna aliye chukuliwa hatua
Yani kodi kila sehemu nabado mnakopa dayle
Bandari mmemuuzia mwarabu na mkataba ni wamile
Najiuliza mungu why
Ulimchukua john mapema ulimchukua tujifunze au tupate kukema
Huu mtihani haki ya mungu mi nakosa chakusema
Kazi yako haina makosa ikikupendeza chakuwa na hawa
Media za bongo zime stuck hazima tena ubunifu
Hazikuzi presenter wapya, zinaangalia nani maarufu
Na hao maarufu sasa kama machangudoa
Mwenye kisu kikali huyo ndiyo utakae ming’oa
Amkeni ninyi hakuna elimu ya bure
Nacho jua me elimu ni ghalama
Siku zote ninach amini cha bure hakina maana
Wanatupa elimu mbovu ya bure isiyo na maana
Na ndo maana siku izi tuna wasomi wajinga sana
Promo ya mama nikubwa kuliko hata utendaji wake

Mabango kila kona akinadiwa, na chawa wake
Wana mdanganya ndege bora kuliko ongezeko la mshahara
Wanamshauri aongeze ndege shilika linaendesha kwahasara
Ukiwachukua viongozi wetu wakaiyongoze marekan
Na wa marekani waiongoze Tanzania
Baada ya miaka 5 marekani itafulia
Ukweli ni kwamba watarudi kuomba msaada Tanzania

Tumefunbua macho, nabado hatuoni
Upepo ni mkali jahazi lazama
Safari bado ndefuu
Tutashinda ila inataka imani, tutavuka jangwani
Kufika nchi ya ahadi, bado mbali sana
Bado mbali sana, bado mbali sana
Sana ooh sana

Nisha tafuta kazi, ya elimu yangu nikakosa
Nikatafuta kazi ya mshahara mdogo nikakosa
Hata ya mshahara wa chakula, bado nayo nikakosa
Nipo na vyeti, nangoja miujiza ya mwamposa
Tatizo wasomi wengi, na waliyo fanikiwa hawapendi siasa
Wajinga ndiyo wanakimbilia, tunapata viongozi wajinga
Uchumi unayumba, bongo akili ndogo inaendesha akili kurwa
Viongozi ni panya road,walovishwa suti
Na sisi walipa kodi tunawapigia saluti
Nchi imejaa migodi ila tunaongoza kwa dhiki
Wanatuuliza mbona atuogi na maji walikata wiki
Nyie niwajing sijawatusi, ila nyie niwashenzi
Mnatuteka tulipo sema ni wezi amtekelezi
Na mama ikikupendeza kuhusu mkataba wa bandari
Usiishie bara peleka na zanzibar
Mnauza twiga bado msigwa anatupanga mpaka basi
Wabunge kututetea na ukimya umepaki basi
Nguvu kubwa inayo tumika kumpamba mitandaoni
Na kwenye media ila huku mtaani
Hakubaliki na pia hauziki
Endeleeni na tenzi zenu zakupeana kila wiki
Na bunge lenu la mchongo, spika wa mchongo
Lumebaki jina la bunge na vikao vya CCM

Tumefunbua macho, nabado hatuoni
Upepo ni mkali jahazi lazama
Safari bado ndefuu
Tutashinda ila inataka imani, tutavuka jangwani
Kufika nchi ya ahadi, bado mbali sana
Bado mbali sana, bado mbali sana
Sana ooh sana

Aya tuache masihala, tuludi kwenye ukweli
Ivi tunako elekea tunafaulu au tunafeli
Miaka miwili tu iliyo pita, tuliishi kwa nguvu ya buku
Na ilo buku unachagua unga kilo au mchele musu
Na sasa mfumuko wa bei, ni zaidi ya mara tatu
Unga kilo buku mbiu, na mchele ni buku tatu
Hapa tu ndo namkumbuka aliye semaga tutamkubuka
Okay tuachane na hilo, kuna kasumba imezuka
Sipendi unafki na uchawa, si mlisema haki sawa
Mbona sasa akikosolewa, mnaleta mambo ya jinsia
Haitoshi wanao kosoa na kesi mnawafungulia
Nawaona tu mnapotea, nawakati mnaijua njia
Mnauza twiga bado msigwa anatupanga mpaka basi
Wabunge kututetea, na ukimya umepaki basi aah
Amakeni nyinyi hakuna elimu ya bure
Nacho jua me elimu ni ghalama
Siku zote ninach amini cha bure hakina maana
Wanatupa elimu mbovu ya bure isiyo na maana
Na ndo maana siku izi tuna wasomi wajinga sana

Tumefunbua macho, nabado hatuoni
Upepo ni mkali jahazi lazama
Safari bado ndefuu
Tutashinda ila inataka imani, tutavuka jangwani
Kufika nchi ya ahadi, bado mbali sana
Bado mbali sana, bado mbali sana
Sana ooh sana

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2023


Album : Amkeni (Single)


Copyright : ©2022 Free Nation.All rights reserved.


Added By : Farida

SEE ALSO

AUTHOR

NAY WA MITEGO

Tanzania

Emmanuel Elibariki, popularly known as Nay Wa Mitego, or simply  Mr Nay,  is a Tanzanian r ...

YOU MAY ALSO LIKE