Home Search Countries Albums

Twende

NACHA

Twende Lyrics


Hakuna kitu kibaya kama hii money
Imefanya washkaji wengi wauwane
"nyasubi ndani ya mbanyu"

Ilikuwa yani daily haso,kuvuja jasho
Kuamka asubuhi kwenye michakato
Mambo bado,haso haso
Usipopambana utakula macho

Unajiona mpweke unabaki wewe
Unakuwa na wasi kama kifaranga kamuona mwewe
Hakuna msaada unaopata ni wao wenyewe
Mpaka unahisi hii dunia kama hujaumbiwa wewe eeh
Kichwa kinauma yani daily vioja
Home hakueleweki halafu mlo ni mmoja
Shida zimejaa unaweza hisi umerogwa
Si tukakomaa si tukajikongoja
Hatukuwahi kukata tamaa tukapambana
Mambo yakajipa haswaa tulitukanwa
Watu wakatuona mafala tukasemwa na
Tukapewa hifadhi tulikuwa hatuna pakukaa
No matter what, usiache kutabasam
Kwetu machungu kwa wengine maisha ni matam
Subira yavuta heri niamini
Amini ukiamini unapata

Kwahiyo achaga uzembe
Kazana ku-push
Tunapita hata mkituwekea vifusi
Kama wembe tu
Mbele nyuma kus
Na town huwa inaendeshwa na wa bush
Sasa twende
Twende twende twende
Nasema twende
Twende twende twende
Sasa twende

Mara ngapi umeanguka sio
Haijalishi mara ngapi umeangua kilio
Haijalishi wako wapi ambao ulihisi kimbilio
Mara ngapi ulitaka piga na huna salio aah
Usitamani cha mwenzako hio mbaya
Washkaji kibao washaishia tu pabaya
Njaa na tamaa,usione maisha haya
Ni mbaya unaweza ishia ushoga na umalaya
Aah binadam ukiwaendekeza utayumba
Utakosa mavumba,utahisi labda ndumba
Na ukiwatangazia shida watavunga
Watakuona mtumba,umechoka umeyumba
Kwanini uwe mnyonge una nguvu una afya
Usije chukia hata mwenzako akipata
Tafuta utapata,ukikosa pambana
Ukipata kidogo shukuru kazana
Usiwape chance ya kukuona una dhiki
Nje wachekee kalie ndani ndo fiti
Unalala chini afu mwanao ana kivitz
Usitie unyonge so pambana kama sisi
Usione mjini wana shine na maisha
Vidume kibao huku mjini wanainamishwa
Nyumba nzuri,gari zuri oya so poa
Oya oya aaah oya

Kwahiyo achaga uzembe
Kazana ku-push
Tunapita hata mkituwekea vifusi
Kama wembe tu
Mbele nyuma kus
Na town huwa inaendeshwa na wa bush
Sasa twende
Twende twende twende
Nasema twende
Twende twende twende

No matter what usiache kutabasam
Kwa wengine maisha ni matam
Subira yavuta heri niamini
Amini,ukiamini unapata
Sasa twende
Twende
Nasema twende
Twende
Sasa twende
Twende
Nasema twende
Twende

Eeeh twende kushoto,twende kulia
Twende kushoto nasema twende kulia
Twende kushoto,twende kulia

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2022


Album : Twende (Single)


Added By : Farida

SEE ALSO

AUTHOR

NACHA

Tanzania

Nacha Ousam is a musician from Tanzania. ...

YOU MAY ALSO LIKE