Home Search Countries Albums

Nasimama

NACHA

Nasimama Lyrics


Kuna vita skuviona sikuepo enzi zile
Vita vya dunia maji maji Kinjeketile
Vita ya mwafrika na mkoloni niliskiaga
Vita ya Tanganyika na nduli Amin Dada

Tutoke huko tuongelee vita vya sasa
Matumizi ya ubabe kwenye madaraka
Sio vichana wala msiwatukane bure
Wanaposema kuwa ngoma za Nacha zitumike shule

Moyo mchafu kuoshea sabuni
Ni kutegemea ukali wa wembe kuipasua kuni
Kumkosoa boss wako ni kutia mchanga ugali huo
Yaani ni kuning'inia kwenye kamba kuanikia nguo

Nawastaajabu vita vya mamba mnamtegemea kenge
Maana ni nadra sana mbuzi kuzaa mende 
Lahaula maana ni vita sugu
Na mkumbuke kicheko na kilio ni ndugu

Nasimama wima nasimama wima
Na kipima race
Maana umasikini, maradhi ndio vita vya kuogopa
Ujinga kichwani umeshaota 

Haya kamata jembe, kamata shoka 
Shambani ndo utajiri unapotoka
Shika panga na jembe tukasake pembejeo
Tupige vita hivi usipige mkeo

Sina uridhi wa viatu niko peku
Ninafunza nashangaa 
Maana niliskia mcheza kwa hutunzwa
Kuwawashia taa vipofu wasione giza
Ni sawa na kususia uchaguzi sioni tija

La hasha mguji kwenye bukta
Yeye ni hatari ndo hao wanaopeleka sheli buta
Mili mikubwa ila akili hazijakua
Maana mnamtupa samaki kwenye maji ili kumuua

Naishi kwenye vioo chonde msipige mawe
Ukimshindwa adui usione aibu ungana naye
Ndio suruali sio kaptula
Hakuna umoja wenye njaa akitokea mwenye chakula

Wamedukia na walichimba wao kisima
Hawakujua Nuhu wa Shilole sio Nuhu wa safina
Kukosea na ukachukia kutukanwa
Ni kulazimisha kupitisha paka njia za panya

Nasimama wima nasimama wima
Na kipima race
Maana umasikini, maradhi ndio vita vya kuogopa
Ujinga kichwani umeshaota 

Haya kamata jembe, kamata shoka 
Shambani ndo utajiri unapotoka
Shika panga na jembe tukasake pembejeo
Tupige vita hivi usipige mkeo

Kumfuta tongo tongo kipofu alafu useme Yes
Ni sawa na kufosi kumpa jina nameless
Wanaona wivu ila cha ajabu hawaoni haya
Eti uvumilivu na busara pia una expire date

Tulikosea wenyewe but ndugu kuwa wapole 
Mnataka amani ya ndoa na mlioa kwa mtogole
Na vita ni kubwa mtapiga sana miayo
Na msitegemee kushinda kurefa ni kaka yao

Inahitaji akili kuzielewa hizi tungo
Vinginevyo utakunja sura kama mgonjwa wa tumbo
Yaani nampoteza mbwa kwa mingi miluzi
Alafu nashinda kila siku ka na mjomba tume ya uchaguzi

Kupiga vita maadili ni kutoona hayo maboya
Wakati kila siku Insta naona mapaja ya Uwoya
Sasa natoa tamko wakimwagika nawaokota
Nawapanda nawatia mbolea wanaota

Nasimama wima nasimama wima
Na kipima race
Maana umasikini, maradhi ndio vita vya kuogopa
Ujinga kichwani umeshaota 

Haya kamata jembe, kamata shoka 
Shambani ndo utajiri unapotoka
Shika panga na jembe tukasake pembejeo
Tupige vita hivi usipige mkeo

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2020


Album : Nasimama (Single)


Copyright : (c) 2020


Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

NACHA

Tanzania

Nacha Ousam is a musician from Tanzania. ...

YOU MAY ALSO LIKE