Pokea Lyrics
Pokea shukurani zangu pokea
Pokea shukurani zangu pokea
Pokea shukurani zangu pokea
Pokea shukurani zangu pokea
Machozi yananitoka
Nikiketi chini nifikirie
Umbali nilikotoka
Hata sijui ni vipi nisimulie(aaah)
Mwema, umekuwa mwema kwangu
Tena umekuwa nguzo yangu wee
Umenifunza subira
Ukanizingira kando na kando
Ah tena wanisikia
Nikianguka waniinua eeeh(aaah)
Sasa mahitaji naweka kando
Sijasahau mema
Na ningependa ujue
Vile moyo unafurahishwa na we
Oooh, maneno yananiishia aah
Umenishangaza kwa matendo yako
Vile wanikumbatia aah
Sina lingine
Lilobakia ni
Pokea shukurani zangu pokea
Sina budi nikwambie
Pokea shukurani zangu pokea
Kwa uaminifu wako
Pokea shukurani zangu pokea
Kwa matendo yako makuu
Pokea shukurani zangu pokea
Ni wewe ulinifunza
Ati shida ni mtumwa wangu
Tena ukanifanya
Mwana ndani ya ufalme wako
Neno lako ni taa
Hata kwa giza nimulikiwe
Tena wewe ni jiwe
Nikianguka nishikiliwe
Matendo yako yameninyamazisha
Siwezi laumu
Mkono wako wa kiume
Umenishindia magumu
Eeeh, na kila mara wanikumbuka
Kwa mipango yako miema
Eeeh yale mabaya waniondolea
Unaniwazia mema
Oooh, maneno yananiishia aah
Umenishangaza kwa matendo yako
Vile wanikumbatia aah
Sina lingine
Lilobakia ni
Pokea shukurani zangu pokea
Sina budi nikwambie
Pokea shukurani zangu pokea
Kwa uaminifu wako
Pokea shukurani zangu pokea
Kwa matendo yako makuu
Pokea shukurani zangu pokea
WATCH VIDEO
ABOUT THIS SONG
Release Year : 2019
Album : Pokea (Single)
Copyright : All rights to the owner.
Added By : Huntyr Kelx
SEE ALSO
AUTHOR
JANET OTIENO
Kenya
Janet Otieno is a Kenyan Gospel Music Singer and Songwriter. She was born in Kisumu, Kenya, the seco ...
YOU MAY ALSO LIKE