Home Search Countries Albums
Read en Translation

Lala Salama Magufuli Lyrics


[Mbosso]
Nalifuta chozi kushoto
Kulia latiririka
Maumivu moyo wa moto 
Nafsi yatatarika

Vilio wakubwa watoto
Viyowe zinasikikika
Wachonge zetu changamoto
Wapi zitashikika

[Christina Shusho]
Umelala iyoo, baba umelala wee
Nenda we Magufuli nenda wee
Tulikupenda Mungu kakupenda zaidi
Baba nenda wee, baba nenda wee

[Jux]
Yaani baba (Baba)
Tutakukumbuka kwa mazuri yako
Sema baba (Baba)
Tutakukumbuka kwa upendo wako

[Madee]
Kuna Muda nalega nakosa power
Nasema no God hii sio sawa
Mbona kuna wengi tu walipaswa kwenda
Unajibu "NO" huyu niliyempenda

Umempenda John, umemchukua John
Umetuacha hatuoni sio alfajiri sio jioni
Tukifikicha mboni kule mbele hatuoni
Mungu akulaze baba mahali pema peponi

[Joel Lwaga & Diamond Platnumz]
Kweli vyema havidumu 
Ni machozi na uchungu
Ni ghafla, ni ghafla
Asante kwa kujenga Tanzania imara
Nenda, nenda, nenda ulale

Ulale salama, pumzika baba
Ulale salama, kazi umeifanya
Ulale salama, tutakuenzi daima
Ulale salama

[Zuchu]
Huzuni imetawala
Jembe Tanzania limetutoka
Yaani kama masihara leo taifa tunahuzunika
Baba uende salama, tutakukumbuka sana
Akupake Maaulana Amina

[Benpol]
Miundo mbinu tunaona (Ona)
Elimu bure tunasoma (Soma)
Makao makuu kwetu Dodoma
Umetupa heshima baba

[Malkia Karen]
Eti njia yetu ni moja
Umetanguli si tunafuatia
Tunajikongoja taifa laumia 
Tunakulilia

[Baba Levo]
Kiumbe jasiri tena mahiri
Ametutoka (Ametutuka)
Jasiri mwenye akili
Ametutoka (Ametutoka)
Magufuli wewe ameondoka
Simanzi Tanzania ametutoka

[Mrisho Mpoto]
Ina maana mapambano kikomo ndio imefikia
Vuta nikuvute historia inakwenda kubakia
Kila ulimi kifafa umeshikwa
Hauwezi kusema hauwezi kuteta
Daima ulisema tukuombee
Ah, ila mauti yamevikwa taji dhidi ya dua
Daima tutakukumbuka 

[Rayvanny]
Jioni jua limezama 
Umetangulia ulale salama
Kila ulosema limetimia
Serekali Dodoma imehamia
Baba mbona hujasubiria
Ikulu ulojenga mwenyewe hujaingia

Ulale, ulale salama
Ulale salama, ulale salama
Ula ula ulale, ulale salama
Ulale salama (Ulale baba)

Lala, lala
Lala lala
Lala lala

[G Nako]
Kilio ukiskie kwa jirani 
Machozi machozi nani afute nani?
Kifo kifo, kifo kifo
Kifo fumbo kubwa duniani

[Lava Lava]
Ni mengi ulituhusia
Upendo mimi na yule
Elimu bora ukatupatia
Watoto waende shule

Tuchape kazi ukasisitizia
Tusikae bure
Mbona sasa umetukimbia
Umetuacha na simanzi baba

[Darassa]
Mungu ana njia zake huwezi hata kumuotea
Mungu anachukua hata unachokinyenyekea
Unachotegemea nguzo yako kuegemea
Ndio maana dini zinasema tuishi kwa ku prepare

Look alas, now we breathe like there is no air
Should I continue singing?
Or let me pray for better days to come
Rest in Peace uncle Magu till we meet again Amen

[Producer Rash Don Boss]
Umetutoa kwenye sifuri mpaka uchumi wa kati
Madaraja babara nzuri ona mwendo kasi

[Khadija Kopa]
Wanawake umetusimamia
Kwenye sekta mbalimbali
Umetusimamisha umetuinua

Ulivyomteua Samia
Umetupa ujasiri tupambane
Asante Magufuli

[Belle 9]
Kila saa uliimaliza migogoro
Njoo uuzindue mradi wako Morogoro
Baba (Baba) Baba (Baba)

Hivi sivyo tulivyotegemea
Imeanguka nguzo tuloegemea
Baba (Baba) Baba (Baba)

Ulale Salama
Ulale salama, ulale salama
Asante kwa wema wako
Ulale salama, asante kwa wema wako
Ulale salama

[Queen Darleen]
Matibabu bure kwa watoto na wazee
Hukutuacha nyuma wanawake twendelee

[Marioo]
Atufute nani machozi 
Taifa lakulilia
Atatuvusha nani mwokozi
Na nahodha umetangulia

Yametutawala majonzi
Baba umetukimbia
Zimetushafura pozi
Huzuni imetuelemea baba

[Abby Chams]
Nuru yaangaza taifa 
Imekatizwa ghafla
Magufuli baba yetu
Tutakukumbuka daima

Pumzika kwa amani
Is out of faith --
All have left is memories
And --- let go

[Maarifa]
Hukuwa Mungu tujue umetimia
Singeshindwa ubaki wewe 
Ili achukue vichaa mia
Ila kama ambavyo mwewe hachagui kuku
Maiti hachagui sanda na kifo hakichagui mtu

[Barnaba Classic]
Kina mama wenye hali za chini
Bodaboda hali za chini
Raia hali za chini 
Wanakuita Magufuli simama

Najihisi kukata tamaa
Ila inanibidi nikubali
Ila Magufuli simama

Ni mengi uliyotenda kwa ushujaa
Haitoshi ulikuwa mzalendo
Magufuli simama
Uliipigania haki hukubagua watu wala mtu
Magufuli simama

[Dulla Makabila]
Mkombozi wa wanyonge umeenda (Aah umeenda)
Jasiri mtenda haki umeenda (Aah umeenda)
Kipenzi cha wananchi umeenda (Aah umeenda)
Mpenda maendeleo umeenda (Aah)

[Chege]
Baba ulale salama, ulale salama
Daddy ulale salama, ulale salama
Hivi kweli tutacheza tena, ulale salama, ulale salama
Uuu la, ulale salama, ulale salama

[Cyril Kamikaze]
Kiongozi jasiri ambaye alipinga rushwa
Alinyanyua wanyonge pale tu alipoangushwa
Hakuogopa fisadi yeyote yeye alimgusa
Huduma kwa wakati bila hata kuzungushwa
Ona barabara vijijini tunafika
Pumzika peponi chuma daima utakumbukwa 
Ulale salama, uuuuu..

[Diamond Platnumz & Tanzania All Stars]
Ulale salama, ulale salama
Ulale salama, ulale salama
Ulale salama, ulale salama
Ulale salama, ulale salama

Ulale salama, ulale salama
Ulale salama, ulale salama
Ulale salama, ulale salama
Ulale salama, ulale salama

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2021


Album : Lala Salama Magufuli (Single)


Copyright : © 2021 WCB Wasafi.


Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

TANZANIA ALL STARS

Tanzania

Tanzania All Stars is a group of artists made up of; Diamond Platnumz, Christina Shusho , Jux , ...

YOU MAY ALSO LIKE