Sitaki Tena Lyrics

Nitachowaambia msiache kumwambia na yeye
Simchukii na na najipa mweyewe oh no
Oh baby sijutiii kuwa mbali naye
Apunguze presha
Mwambieni sililii
Penzi lake nilishalihimisha
Hazijabaki memory wala kumbukumbu
Nilishamsahau mazima
Hata nikimwona namwona ka nungu nungu
Sio kama namvunjia heshima
Makombe amalize ajifushe na nyungu
Akakoge na maji ya kisima
Ila mimi nilisha apa kwa mwenyezi Mungu
Haitojirudia tena
Sitaki tena, tena mwambieni asinisumbue mimi
Sitaki tena, nipo buheri na nafsi yangu
Sitaki tena, abaki na zake nibaki na zangu
Sitaki tena, nipo buheri na nafsi yangu
Dua zake mbaya kwangu nifeli nilipo sasa anajua
Najua likiwa ka kiza kikitanda ananiwaza ananijua
Mwambieni asihangaike na mipasho moyo wake mimi naujua
Sitaki kumdhalilisha nikataja na siri zake nikaamuumbua
Hazijabaki memory wala kumbukumbu
Nilishamsahau mazima
Hata nikimwona namwona ka nungu nungu
Sio kama namvunjia heshima
Makombe amalize ajifushe na nyungu
Akakoge na maji ya kisima
Ila mimi nilisha apa kwa mwenyezi Mungu
Haitojirudia daima
Sitaki tena, tena mwambieni asinisumbue mimi
Sitaki tena, nipo buheri na nafsi yangu
Sitaki tena, abaki na zake nibaki na zangu
Sitaki tena, nipo buheri na nafsi yangu
Mwambieni sijutiii kuwa mbali naye
Apunguze presha
Mwambieni sililii
Penzi lake nilishalihimisha
WATCH VIDEO
ABOUT THIS SONG
Release Year : 2021
Album : Sitaki Tena (Single)
Copyright : (c) 2021
Added By : Huntyr Kelx
SEE ALSO
AUTHOR
YOU MAY ALSO LIKE