Mkombozi Lyrics
Owoo, owoooo
Aaah aah sema na Mola
Aaah bado napolia mama
Eh eh eh eeeh eeeeh
(Tongwe Records)
*Bin Laden*
Napiga goti napiga ishara ya msalaba
Dunia imenipiga kofi namuomba Baba la baba
Nipimie shoti ya bapa nizime mada
Asubuhi nigongee noti niende kuifanya ibada
Nadaiwa kodi ya pango, nadaiwa ada ya watoto
Na mama wa kambo anamchuna baba
Na baba yuko ng'ambo ni mwaka sijaona msaada
Ama kweli dunia ina mambo hadi jogoo anaweza taga
Jirani ananiambia be humble, be humble
Nikipiga kizinga we unafunga mlango
That's ridiculous(Hahaha) it's now funny am serious
Am genius, though inanitesa am notorious
Baba hakutupa uridhi, wa pasi wala feni
Wala peni ambayo ingenipa elimu shuleni
Bali alituachia madeni na sifa ambayo kweni
Sa huyo ndo baba gani? Humble au mtemi?
Na mtaani kuna binti nimempa mimba
Mtoto mgeda muda wote pira litadimba
Na sina dusko so kwa doctor siwezi timba siwezi vimbva
Na kila chocho Bongo wananilinda
Nimekesha kwa waganga
Nimevunja nazi njia panda
Nimeshikishwa tungule msata
Mkata nikambeba manyanga
Mi kesha kinabiii
Nyumba zote za ibada
Nimeshiriki sana
Maana sura kukufuru sijaumbwa nawe
Kumbe yupo Mungu, Mkombozi
Wa kukufuta machozi
Pale unapolia mwana
We baba(Yeiii wowowowo)
Kumbe yupo Mungu, Mkombozi
Wa kukufuta machozi
Pale unapolia mwana
We baba(Yeiii wowowowo)
Nishaiba nikaenda mabusu na ndugu hawakuja niona
Na wakasema hayawahusu mwizi anatakiwa kuchomwa
Nilipotoka nikawabusu wakasema nimewasonya
Nikaona eeh maji mazito kuliko damu ya Roma
Ukiendekeza ndugu, utavuna magugu
Utakufa kidudu na Mungu hutamwabudu
Utamkataa wa joto utamkana wa baridi
Atabakia wa vuguvugu naye pia ataleta gubu
Si campi keto, stressi inaleta furaha freshi
Be passion, anguko kubwa ni kuikosa attention
Its not fair, nawapa proposal they dont care
Na watasema huna demandi fitina watakuekea
Huku nadaiwa vikoba, kule nadaiwa rejesho
Naenda kujificha goba, usiku narudi peko
Nawaza hata kuroga nikiamini nitaipata kesho
Au nisali sala toba nijue nikwepe mateso
Ooh Jesus, fanya miujiza
Naona giza ukija mwanga unaniumiza
So please kama unaskiza naijongea hatari
Useme neno moja tu naahidi nitakesha pale
Nimekesha kwa waganga
Nimevunja nazi njia panda
Nimeshikishwa tungule msata
Mkata nikambeba manyanga
Mi kesha kinabiii
Nyumba zote za ibada
Nimeshiriki sana
Maana sura kukufuru sijaumbwa nawe
Kumbe yupo Mungu, Mkombozi
Wa kukufuta machozi
Pale unapolia mwana
We baba(Yeiii wowowowo)
Kumbe yupo Mungu, Mkombozi
Wa kukufuta machozi
Pale unapolia mwana
We baba(Yeiii wowowowo)
We baba, we mwana
Aah pale unapolia mama
(Eh eh eeh eeeh)
Kumbe yupo Mungu, Mkombozi
Pale unapolia mama
We baba eeeh eeh
Kumbe yupo Mungu, Mkombozi
Pale unapolia mama
We baba eeeh eeh
(Tongwe Records)
*Bin Laden*
WATCH VIDEO
ABOUT THIS SONG
Release Year : 2020
Album : Mkombozi (Single)
Copyright : (c) 2020
Added By : Huntyr Kelx
SEE ALSO
AUTHOR
ROMA
Tanzania
Roma real name Ibrahim Mussa, also known as Roma Mkatoliki is a Tanzanian-USA based artist/rapper/ac ...
YOU MAY ALSO LIKE