Diaspora Lyrics
Tongwe Records Beiby
(Bin Laden)
Umwambie sikupenda, kuikimbia nchi yangu
Kabla kalenda nimeondoka kabla ya mwanangu
Na sijui ninapokwenda na simjui na mrithi wangu
Usije ukambemenda mwanangu oii
Kitovu chake ukizike nilipopitisha unyayo
Akiwa wa kike ndo furaha nitakayo
Ukinizalia dume Inshallah ni hayo
Nitampa jina la mtume na nitamuita Matayo
Akikuwa mwambie babake alikuwa mwanaharakati
Na ukamwonyesha ununio ndio kumbukumbu iliyobaki
Awaheshimu nduguze ambao walimwachia ziwa
Wamdhamini wamtunze abadani asijione mkiwa
Na asinichukie mimi maana sikumchukia babu yake
Akikuwa atajua kwanini na ataheshimu maamuzi yake
Na uchunge ulimi aishike dini yamkini ana jini mkongwe
Na umsikizishe yangu mapini ---
Na ukipata usimsahau mama, mkumbuke na bibi
Niombee nitusue mnyama, nabeba kavu msumbiji
Sijui nitakuona nitakufa sijui nitarudi
Akikuwa mwambie Roma ndo baba we ndo shahidi
Uvumilie, utulie, umlilie
Haya maisha ni safari
Usilie, uvumilie, umtulie na ulilie
Haya maisha ni safari
Nafahamu utazaa kwa uchungu
Leba utalia na mengi yakidondoka chini ya uvungu
Atambeba malaika wengi
Mimba huja na kisirani, na kuna unavyotamani
Kumvukuta sivo mfodhani ila siwezi rudia njiani
Na unafahamu hunnie ile nyumba uridhi haina vigae
So unaweza pima mzani ni budi ama nikomae
Bora nikomae tu tujichange tumjengee mama kibanda
Inshallah mpaka uzae nitakuwa nimejipanga
Na nimetuma picha yangu waonyeshe wanangu wasinisahau
Waambie baba atarudi uwape moyo angalau
Kuna muda nina hamu ya ngono ila sina hamu ya mapenzi
So please ongeza visomo kwa yule Ustadh wa Mbezi
Najua unanimiss ila jitunze nami nitakutunzia fimbo
Walinde wanangu wao ndo warithi na ndizo za Roma simbo
Wananiambia mashabiki Roma rudi uchukue jimbo
Huku ukizingua polisi tu unawekewa goti la shingo
Basi ni hayo tu maisha ni mapambano ila sio sinza
Na usisahau kuwapa tano Dajide, Mada na Siza
Na uwaambie huku watu hawachagui kazi
Ila majungu na umbea yaani vitu ni vingi mzazi
Uvumilie, utulie, umlilie
Haya maisha ni safari
Usilie, uvumilie, umtulie na ulilie
Haya maisha ni safari
Uvumilie, utulie, umlilie
Haya maisha ni safari
Tongwe Records Beiby
(Bin Laden)
WATCH VIDEO
ABOUT THIS SONG
Release Year : 2020
Album : Diaspora (Single)
Copyright : (c) 2020
Added By : Huntyr Kelx
SEE ALSO
AUTHOR
ROMA
Tanzania
Roma real name Ibrahim Mussa, also known as Roma Mkatoliki is a Tanzanian-USA based artist/rapper/ac ...
YOU MAY ALSO LIKE