Neno Lako ni Kweli Lyrics

Ni kweli, ni kweli
Neno lako ni kweli
Ni kweli, ni kweli
Neno lako ni kweli
Nimedhibitisha wala sina mashaka
Neno lako ni kweli
Nimedhibitisha wala sina mashaka
Neno lako ni kweli
Ni kweli, ni kweli
Unaweza ni kweli
Ni kweli, ni kweli
Unaweza ni kweli
Nimedhibitisha wala sina mashaka
Unaweza ni kweli
Nimedhibitisha wala sina mashaka
Unaweza ni kweli
Katikati ya kelele dunia ikitingisika
Wewe ni ngome yangu nitakuwa imara
Wakitangaza mauti unatangaza uzima
Wewe ni ufufuo na uzima
Katikati ya kelele dunia ikitingisika
Wewe ni ngome yangu nitasimama imara
Wakitangaza mauti unatangaza uzima
Wewe ni ufufuo na uzima
Neno lako moja latosha
Kuangamiza jeshi la adui
Na maneno ya wabaya na kuwatupa mbali
Katikati ya giza nene
Elimu na ujuzi vinaposhindwa
Neno lako ni nuru ing'aayo gizani
Wengi wakisema siwezi
Wewe ukisema naweza
Baba neno lako ni kweli
Na hata kama wengi wameshindwa
Na hata CV yangu haieleweki
Kwa neno lako mimi ni mshindi
Nimedhibitisha wala sina mashaka
Neno lako ni kweli
Nimedhibitisha wala sina mashaka
Unaweza ni kweli
Katikati ya jangwa nikiwa na kiu
Wewe wanipa maji mwambani
Katikati ya jangwa mimi nikiona kiu
Wewe wanipa maji mwambani
Hapo mwanzo ulikuwepo
Vyote vilifanyika
Kwa neno lako Mungu
Pasipo neno hakuna chochote
Kilichofanya neno lako ni kweli
Shuhuda zako ni kweli
Wala haudanganyi neno lako ni kweli
Shuhuda zako ni kweli
Wewe haudanganyi neno lako ni kweli
Kwa neno, kwa neno lako mimi ni mshindi
Halleluyah, Halleluyah, Halleluyah Amen
Kwa neno lako nasimama imara
Halleluyah, Halleluyah, Halleluyah Amen
Wewe waona taifa kubwa
Ndani yake aliye tasa
Ulimuita Ibrahimu baba wa mataifa
Akiwa hana mwana ulidhibitisha neno lako
Kwa mwanamke tasa akapata watoto
Ni jambo gani gumu linipate
Hata nisiamini neno lako
Nimelidhibitisha neno lako ni kweli
Wala sina mashaka nakuamini Mungu
Kwa neno, kwa neno lako mimi ni mshindi
Halleluyah, Halleluyah, Halleluyah Amen
Kwa neno lako nasimama imara
Halleluyah, Halleluyah, Halleluyah Amen
WATCH VIDEO
ABOUT THIS SONG
Release Year : 2021
Album : Neno Lako Ni Kweli (Single)
Copyright : (c) 2021
Added By : Huntyr Kelx
SEE ALSO
AUTHOR
EMMANUEL MGOGO
Tanzania
Emmanuel Ezekiel Mgogo is a Tanzanian Gospel Singer born 27th of June in Mbozi. Emanuel Mgogo is bes ...
YOU MAY ALSO LIKE