Mniombee Lyrics

Jua la utosi lachoma
Nimejaribu kufosi nimekoma
Sijui mikosi na homa
Vyote mie
Huenda kafara nililovunja koroma
Nishapiga manyanga na ngoma
Nishazunguka Tanga Kigoma
Mola nisaidie
Eeh kile kidogo nichotuma kipokeeni
Mjini kupata kwa foleni
Sina muda nitarudi ningojeeni
Mniombeee
Vizawadi vingine peleka ukweni
Na utunze siri isiende pembeni
Mtoto akitaka simu namba mpeeni
Naye aongeee
Naogopa pata potea kwenye giza
Kuongea kuigiza
Ila mwambie anitunzie eeh eeh
Zile subiri ngojea nitazimaliza
Nitabebea sitoagiza
Ila mwambie anitunzie ooh ooh
Mniombee, mniombee, mniombee
Nikipata bado kidogo mie natafuta
Mniombee, mniombee, mniombee
Mtoto akikua mwambie baba hajakufa
Mwambie babu na bibi
Nitarudi karibuni
Ila shida zimezidi
Nakosa hata sabuni
Mama ulichoniambia sijakosea
Nisitamanigi cha mtu
Tena nichunge macho kukodolea
Kuchukua nisisubutu
Oooh muda mwingine
Nahisi nina laana
Oooh au nyota haina makali
Naogopa pata potea kwenye giza
Kuongea kuigiza
Ila mwambie anitunzie eeh eeh
Zile subiri ngojea nitazimaliza
Nitabebea sitoagiza
Ila mwambie anitunzie ooh ooh
Mniombee, mniombee, mniombee
Nikipata bado kidogo mie natafuta
Mniombee, mniombee, mniombee
Mtoto akikua mwambie baba hajakufa
WATCH VIDEO
ABOUT THIS SONG
Release Year : 2020
Album : Nipokee/ Mniombee (EP)
Copyright : (c) 2020 Lykos Empire 2020
Added By : Huntyr Kelx
SEE ALSO
AUTHOR
PRODUCER BONGA
Tanzania
Producer Bonga is a Musician | Sound Engineer | Music Producer signed under Lykos empire from Tanzan ...
YOU MAY ALSO LIKE