Home Search Countries Albums

Nyumbani

NIKKI WA PILI Feat. MALLU P, ISAAC

Nyumbani Lyrics


Eeh eeeh
Nyumbani, nyumbani
Kwetu nyumbani
(Machords you killin’it)

Najua kwamba nyumba sio nyumbani
Wasio na nyumba pia wana nyumbani
Na marafiki wanaonijua kiundani
Nikiwa nao bana pia ni nyumbani
Na nyumbani pia ni unyumba
Na nyumbani sio kwa mchumba
Ki arachuga home kwa wajuba
Nyumbani ni upendo wa muumba
Nyumbani ni shuleni na ma teacher
Nyumbani ni michezo kujificha
Nyumbani vitamini ka mchicha
Nyumbani sio mamoshi zima shisha
Wanangu wote shimboni na chicha
Nyumbani huwaga hakuna mkosi
Na mama huwaga hakuna nsosi
Na busu lake juu ya utosi
Kulala sana jumamosi
Nyumbani ni ki boss boss boss
Ha ha ha, boss

Nyumbani, nyumbani
Kwetu nyumbani
Nitaumia sana
Nyumbani, nisiporudi nyumbani
Nyumbani nimepa miss
Nyumbani, nyumbani
Kwetu nyumbani

Familia kubwa kama genge la el chapo
Pozi la nyumbani ni viringi na michapo
Hakuna mkubwa kwa dingi wote vichapo
Mjomba mnoko mafunzo kama tupo chapel
Uncle uncle
Ukishampa hela anakuwa kipenzi chako
Uncle uncle
Na mate ya bibi unajua ndo Baraka zako akutemee
Utaoa linin i shangazi ameingia akusemee
Embe dodo embe dodo dodo
Waite watoto wa mama mdogo mdogo
Wa marehemu baba mdogo mdogo
Enzi zake si kidogo dogo
Kwa kikubwa na kidogo dogo
Alitupenda sio kitoto toto
Alale pema baba mdogo
Nitaumia sana
Nyumbani, nisiporudi nyumbani
Nyumbani nimepa miss
Nyumbani, nyumbani
Kwetu nyumbani
Nyumbani, nyumbani
Kwetu nyumbani
Kwetu nyumbani

Nitaumia sana
Nisiporudi  nyumbani
Nimepa  miss  nyumbani

(Machords you killin’it)

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2021


Album : Nyumbani (Single)


Added By : Farida

SEE ALSO

AUTHOR

NIKKI WA PILI

Tanzania

Nikki wa Pili is an artist from Tanzania. ...

YOU MAY ALSO LIKE