Home Search Countries Albums

Rais wa Kitaa

NAY WA MITEGO

Rais wa Kitaa Lyrics


Niliyesimama mbele yenu sio mbunge ni msanii
Natumia sanaa kuitetea jamii
Naongea nikiwa Bongo sitakimbia kama Roma
Mkiniteka mkinifunga bado dunia itasonga

Nani kamwambia mheshimiwa eti tumekubali tozo
Hapana sio Tanzania labda Zambia au Congo
Makato ni makubwa wananchi wanaumia
Hivi ni kwamba hamskii au ndo mnapuuzia?

Mishahara ya wabunge ni jasho la wananchi
Spika naongea na wewe kwa niaba ya wenye nchi
Kuna wabunge kumi na tisa walishafukuzwa na chama
Chadema ina maana hawana chama

Na bado nao bungeni na wanapokea mshahara
Hivi unatuchukulia aje unatuona bongolala?
Wimbo ulianza taratibu na sasa umepamba moto
Unapendwa na wananchi kwa viongozi kaa la moto

Katiba mpya ni sasa, katiba mpya ni sasa
Wanaoimba ni wananchi pamoja na wanasiasa
Mafuta bei juu, gesi bei juu
Kila kitu bei juu, mtatuua mwaka huu

Sukari imepanda bei
Luku tozo pesa wapi nitakope?
Nani atusemee, semee sisi wanyonge
Wacha niwasemee
Nani atusemee, semee sisi wanyonge
Rais wa Kitaa

Sukari imepanda bei
Luku tozo pesa wapi nitakope?
Shebi huku miriamu wameikataa
Chombo mikokote

Nani atusemee, semee sisi wanyonge
Ni Rais wa Kitaa
Nani atusemee, semee sisi wanyonge
Tusijiite wanyonge hapana nakataa

Mi ni mmoja kati waliosema unaupiga mwingi
Nahisi una makocha wengi watakukosesha vingi
Nilikwambia hawakupendi wameshakuingiza kingi
Wanakitaka hicho kiti wana tamaa hao madingi

Hey wapi na wapi? Nchi ya wapi?
Mpangaji analipa kodi na tozo ya jengo
Huu ni wizi na mnaiba bila kutumia akili
Hivi nani anawashauri, mnajichimbia kaburi

Uchumi hukua kwenyu kwa wananchi sufuri
Siku hazigandi ni swala tu la muda
Acha iendelee kunyesha tuone panapo vuja

Oyaa wanangu wee, Corona kweli ipo
Nawa mikono vaa barakoa kwenye mkusanyiko
Nchi na mambo hii yataka moyo kuwa mpinzani
Yaani unabambikiwa kesi na unasota gerezani

Mnajenga mimba za chuku hamjifunzi kwa majirani
Mbunge lenyewe chama kimoja si mfute tu upinzani
Mbaki wenyewe tusitafute mchawi nani?

Sukari imepanda bei
Luku tozo pesa wapi nitakope?
Nani atusemee, semee sisi wanyonge
Wacha niwasemee
Nani atusemee, semee sisi wanyonge
Rais wa Kitaa

Sukari imepanda bei
Luku tozo pesa wapi nitakope?
Shebi huku miriamu wameikataa
Chombo mikokote

Nani atusemee, semee sisi wanyonge
Nani atusemee, semee sisi wanyonge

Hii ni tozo babu kubwa, babu kubwa
Au sio wanangu sema babu kubwa
'Tozo babu kubwa'

Hii ni tozo babu kubwa, babu kubwa
Au sio wanangu sema babu kubwa
'Tozo babu kubwa'

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2021


Album : Rais wa Kitaa (Single)


Copyright : (c) 2021


Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

NAY WA MITEGO

Tanzania

Emmanuel Elibariki, popularly known as Nay Wa Mitego, or simply  Mr Nay,  is a Tanzanian r ...

YOU MAY ALSO LIKE