Home Search Countries Albums

Hatufanani

MARTHA MWAIPAJA

Hatufanani Lyrics


Oooh, ooh ooh...
Hatufanani, hatufanani
Kuna neema inanibeba mimi, hatufanani
Hatufanani, hatutafanana
Kila mtu na neema yake, hatufanani

Hatufanani, hatutafanana
Kila mtu na neema yake, hatufanani
Hatulingani, hatutalingana
Kila mtu na neema yake, rafiki, hatufanani

Kwa Neema ya Kristo tunaendelea mbali

Nimetoka mbali mimi hakuna aliyejua niliyopitia
Iligharimu Mungu aje anisaidie, mimi kuwa salama
Iligharimu Mungu ashuke aniambie neema iko na wewe
Nililalamika kwa Mungu kwa nini magumu yanipate mimi

Nikasema nimekosa mimi sana, mbona kila siku nalia mwenyewe tu
Nikasema kwa nini na yule aliye kama mimi
Nikalalamika nikasema kila siku ni mimi ninayeteseka
Iligharimu Mungu aje kwangu aniambie Mwanangu ipo neema
Kwa upole akaniambia wanadamu hamtafanana
Nikasikia natiwa nguvu kwamba wote hatutafanana

Hatufanani, hatutafanana
Kila mtu na neema yake, hatufanani
Hatulingani, hatutalingana
Kila mtu na neema yake hatufanani

Hatufanani, hatutafanana
Kuna neema inanibeba mimi, hatufanani
Hatulingani, hatutalingana
Kila mtu na neema yake wewe, hatufanani

Hatutafanana, mimi na wewe
Ni neema tu inatusaidia
Mungu peke yake ametusaidia

Ninashukuru kwa Mungu wangu hatazami kama mwanadamu
Ninashukuru kwa Yesu wangu hachagui nani amsaidie
Mnionavyo ni Mungu tu, sijatoka hapa rafiki huh
Nimetembea kutoka mbali, usinikasirikie mwenzio
Usitake nianguke chini, kuna neema inanisaidia hatufanani
Usichimbe shimo nitumbukie, kuna nguvu imenivusha kule hatufanani
Ungepewa neema ujue nilikotoka, ungesema kweli hatutofanani

Hatufanani rafiki, neema yangu na yako si sawa
Usinipangie mabaya kwa siri, kuna neema imenisaidia
Mimi nawe hatufanani neema yangu tu imenisaidia
Hatufanani rafiki tusichukiane, kila mtu na neema yake tu
Hatufanani

Hatufanani, hatutafanana
Kila mtu na neema yake, hatufanani
Hatulingani, hatutalingana
Kila mtu na neema yake hatufanani

Hatufanani, hatutafanana
Kuna neema inanibeba mimi, hatufanani
Hatulingani, hatutalingana
Kila mtu na neema yake wewe, hatufanani

Kwa mkono wa Mungu tunaendelea
Kamwe hatutafanana haa
Asante kwa Mungu wangu
Asante kwa Yesu wangu
Anayetusaidia Halleluyah

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2021


Album : Hatufanani (Single)


Copyright : (c) 2021


Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

MARTHA MWAIPAJA

Tanzania

Martha Mwaipaja is an influential Gospel Singer hailing from Tanzania in East Africa, and recognized ...

YOU MAY ALSO LIKE