Maneno Lyrics
(Kimambo on the beats)
Nimezaliwa vuguruni
Miaka kadhaa imepita
Maisha ya hali duni
Nikahisi kuvunjika moyo
Kusota barabarani
Baba na mama malapa
Kuchekwa na majirani
Nusura nivunjike moyo
Mungu si adhumani
Akanipandisha cheo
Nikaitwa na Rayvanny
Tukashoot na video
Kiutani utani
Ukawa ndo ufunguo
Mara nikadate na fulani mmmh
Matusi kutukanwa
Na visa vyote visanga navumilia
Mengine yananichoma
Hadi yanafanya mwenzenu najililia
Mi bado mdogo sana
Mengine nashindwa kuvumilia
Kipi nimefanya kibaya
Mpaka mwenzenu nang'ang'aniwa
Aaah, maana ni mengi kutwa kucha nasikia
Ati kuimba siwezi sawa nishazoea
Aaah, maana ni mengi kutwa kucha wanaongea
Yatakauka machozi nami nitatulia
Sababu gani we rehani
Nipoteze nilichokitafuta
Kwa nia gani ya dhamani
Fadhila haishindwi kukumbuka
Niwaambie mimi sipati mimi
Kuwepo hapa nilipo
Niombee yaaani mzazi wangu
Kokote huko mliko
Wote wametangulia
Walonileta kwa dunia
Nimebaki peke yangu angalia
Mmmh
Dua njema sasa ninawaombea
Mengi nakumbuka ninalia
Mpaka maumivu yananizidia
Mmmh
Matusi kutukanwa
Na visa vyote visanga navumilia
Mengine yananichoma
Hadi yanafanya mwenzenu najililia
Mi bado mdogo sana
Mengine nashindwa kuvumilia
Kipi nimefanya kibaya
Mpaka mwenzenu nang'ang'aniwa
Aaah, maana ni mengi kutwa kucha nasikia
Ati kuimba siwezi sawa nishazoea
Aaah, maana ni mengi kutwa kucha wanaongea
Yatakauka machozi nami nitatulia
WATCH VIDEO
ABOUT THIS SONG
Release Year : 2020
Album : Maneno (Single)
Copyright : (c) 2020
Added By : Huntyr Kelx
SEE ALSO
AUTHOR
YOU MAY ALSO LIKE