Lala Salama (Magufuli) Lyrics
Bwana Mungu nashangaa kabisa
Nikitazama jinsi ulivyo
Unawachukua wapenda tunaowapenda
Na tukiwapenda unawapenda zaidi
Jina lako lihimidiwe
Nayaona machozi ya wanyonge
Uliowatetea wanakulilia
Lala salama Dr John Pombe Magufuli
Safari njema malaika wa Mungu akupokee salama
Mungu umlaze rais wetu wa Tanzania (Mahali pema)
Kipenzi cha watanzania
Umlaze rais wetu wa Tanzania (Mahali pema)
Shujaa wa Afrika
Nchi yangu imezizima kila kitu kimesimama (Simama)
Watu wote tunakulilia, na tuna huzuni mioyoni
Umeitikia wito wa Mungu baba aliyekuumba
Watanzania tukiwa bado tunakuhitaji
Ni vile kazi ya Mola hainaga makosa
Lala salama Shujaa wa Afrika
John Pombe Magufuli kipenzi cha watanzania
Na wasio pia watanzania
Umeacha alama mioyoni mwetu watanzania
Na africa kwa ujumla
Bwana ametoa lakini bwana ametwaa pia
Jina la Bwana libarikiwe AMEN
Lala salama, salama
Safari njema, safari njema
Mungu umlaze rais wetu wa Tanzania (Mahali pema)
Kipenzi cha watanzania
Umlaze rais wetu wa Tanzania (Mahali pema)
Shujaa wa Afrika
WATCH VIDEO
ABOUT THIS SONG
Release Year : 2021
Album : Lala Salama (Magufuli) (Single)
Copyright : (c) 2021 The VOA
Added By : Huntyr Kelx
SEE ALSO
AUTHOR
LINEX SUNDAY MJEDA
Tanzania
Linex Sunday Mjeda is a bongo flavour artist from Tanzania. ...
YOU MAY ALSO LIKE