Home Search Countries Albums

Hujambo Mwanangu

ROSTAM Feat. FEROOZ

Hujambo Mwanangu Lyrics


It's Rostam baby
Maa...(Tongwe Records bby)
Bin Laden

Nakusalimia kwa jina la jamhuri ya Tanzania 
Siku nyingi hatujaongea na sisi ni familia
Na mbona hukuja kumzika baba, kwa nini?
Ukipata muda kasome Luka 9 mstari wa 60
We nae umezidi utukutu ndio maana baba alikuchukia
Wengi tulioko huku mioyo yetu iliumia 
Kuona baba akiwakemea waliotuonea aliwasifia
Mwenzangu ulipendwa sana, nyimbo zako alifurahia

Ulideka ulipewa zawadi ya t-shirt na kofia
Kaka marehemu hasemwi njoo tujenge familia
Acha niondoke nina damu ya kunguni nisije nikajifia
Tunaimba wote nafungiwa mimi? Umesahau ya kibamia?

Ila sasa unaweza ukarudi (Mmh) 
Mbona mambo yako shwari (No)
Hata kaka aliyekuwa hakupendi 
Mambo yake yako mshazali (Wacha)
Aliuza nyumba ya kino bila hela ya udalali 
Akapata ya Kigamboni kasombwa na upepo wa bahari

Hii ni hatari kuna watu baba aliwapa kiburi 
Tulionekana wajeuri kila tulipo mshauri
Eh eh kaka eeh basi rudi ufukue kaburi
No na wasiwasi na walio baki mama awaangalie vizuri
Kama? Kaka yetu aliye hai na yuko happy? Yule chenga
Polepole haya mambo sasa ni msiba 
Njoo chemba (Narudi Januari na nitafika kwa kaka Bumbuli)
Hata kwa mamdogo yule mwalimu wa tanga utaishi vizuri
 
Mama tuna kutazama we
Mama tufute machozi
Mama mama mama 
Rudisha tabasamu
 
Kila mtu anasema lake hivi kipi kime muua baba?
Achana na maneno ya watu na tena badirisha mada
Ni maradhi ya moyo usisikilize hizo kelele 
Muache baba apumzike kwenye nyumba ya milele
Okay, na mama anaendeleaje yuko Dar au yupo mkoa?
Tafadhali msisitize asiache kuvaa barakoa
Mama yako yupo majukumu ndio yamembana
Na juzi kwenye kikoba wamempa uwenyekiti wa chama
Na nimewapenda sana wale wasaidizi alio wachagua 
Waliopita ni wezi wa vikoba yani afadhali amewatimua
Na kikoba cha vijana bado anakiongoza kaka
Mmh yule sidhani kama mama atamuacha nina mashaka

Hivi vipi huko umeshaonana na dada? 
Maana hata yeye ilikuwa haziivi na baba
Dada amechoka wanafamilia wana mwangusha
Ila nitaonana nae sisi ni ndugu siwezi kumsusa
Shauri zenu bwana tukipewa urithi msishangae
Nyie si mmegoma kurudi tusilaumiane baadae
Emhee yani toka nikujue leo mdio umeongea cha maana
Nina mengi ya kukuuliza smije mkamdhulumu mama

Vipi swimming pool ya babu ile ya Rufiji?
Sasa hivi iko chini ya nani na inamnufaisha bibi?
Baba alisimamia katuachia sisi wanae 
Na kumewekwa mataa yanayo imulika Kisarawe
Na ile biashara ya Bagamoyo baba alioisitisha?
Juzi mjomba alisema iendelee inasikitisha
Kwa  hiyo kamsaliti baba eh? Ah ah sijamaanisha
Mama amuwangalie kaka yake kwa makini atamfelisha
 
Mama tuna kutazama we
Mama tufute machozi
Mama mama mama 
Rudisha tabasamu
 
Baba alifanya mema mengi muacheni alale
Oya saa ngapi huko? Unasikiliza ngoma za kale?
Natamani kuisikiliza ya kwelina kwenye daraja la Mfugale
Huku saa 8 nina mawazo hivi njiwa bado wapo wale?
Njiwa wametutia hasara sijui aliwaza nini baba?
Kivipi? Wakati naondoka mi niliwaacha wako saba
(Mama akaongeza watatu) njiwa mkubwa hatagi kwa nini?
Lile banda kule kijijini sa baba alilijengea nini?
Ila nitunzie sana mamangu bado ulinzi anauhitaji na kingine 
(Mwe makini na yule baba mdogo mchungaji)

Mama yupo sehemu salama usijali punguza uwoga 
Na ushauri pia anapewa na baba mkubwa wa Msoga
Halafu baba na yule Uncle wa Singida hawakupatana 
Kwa nini wasikae wamalize tu tofauti zao na mama 
Ndio uongee nae sasa harudi si unajua kuwa alihama 
Yeye  na rafiki zake wapate usalama
Na wale nashangazi wawili bado wana hasira na baba
Wangesamehe na kusahau wangempa mama msaada
Na umwambie mama aendelee kushirikiana na majirani
Familia ina amani waliokwazwa warudi nyumbani

Naona kikao cha familia kina ndugu wa upande mmoja 
Uncle anawajibu ndugu wa nje na kuacha kujadili hoja
Ebu kwanza ngoja mama anaingia tutaongea baadaye 
Nitakucheki ngoja nimpe simu uongee nae

"Halloo hujambo mwanangu...."

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2021


Album : Hujambo Mwanangu (Single)


Copyright : (c) 2021


Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

ROSTAM

Tanzania

ROSTAM  is a music group made up of two tanzanian rappers ROMa and Stamina. ...

YOU MAY ALSO LIKE