Home Search Countries Albums

Fungu Lyrics


Yaani kufunga na kufungua 
Ukabeba kilicho chako
Umeniongezea maumivu 
Walonionyesha wenzako

Umepepea na furaha 
Ya mtoto wa mwanamke mwenzako
Ukaniweka rahani kisa
Penzi la kunicherehani

Na hata nikijishusha unakuja juu
Imekuwa nongwa unaongea kikuu
Nilisimama kifua mbele kama sina tatizo nawe
Kumbe ninakulia ndani niache nijiishie eeh

Labda haukuwa riziki yangu
Kama na fungu langu ananipokonya
Wacha niyaone mwenyewe
Mbona hata mama ameshanikanya
(Labda alikuwa fungu langu)
(Oooh labda)

Labda haukuwa riziki yangu
Kama na fungu langu ananipokonya
Wacha niyaone mwenyewe
Mbona hata mama ameshanikanya
(Alishanikanya mama sikutaka kusikia)
(Ayayaya)

Penzi limekuwa matapishi 
Linanuka ng'onda
Nilijifanya mbishi
Leo naunguza donda

Mi napalilia mapishi
Wenzangu wanaonja
Maibilisi 
Wazima na wagonjwa

Kama ungeniweka wazi
Mapema tungeachana
Moyo ushakufa ngazi
Kwa kupigwa dana dana

Kutwa nina simanzi
Nishakata taama
Natamani nijitie kitanzi
Nisikuone mama

Nilisimama kifua mbele
Kama sina tatizo nawe
Kumbe naukunia ndani

Kulakoloze kwa vyozevyo, wa ngoze
Kulakoloze chane 

Labda haukuwa riziki yangu
Kama na fungu langu ananipokonya
Wacha niyaone mwenyewe
Mbona hata mama ameshanikanya
(Labda alikuwa fungu langu)
(Oooh labda)

Labda haukuwa riziki yangu
Kama na fungu langu ananipokonya
Wacha niyaone mwenyewe
Mbona hata mama ameshanikanya
(Alishanikanya mama sikutaka kusikia)
(Ayayaya)

Wacha niyaone mwenyewe....

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2020


Album : Fungu (Single)


Copyright : (c) 2020 VOA


Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

LINEX SUNDAY MJEDA

Tanzania

Linex Sunday Mjeda is a bongo flavour artist from Tanzania. ...

YOU MAY ALSO LIKE