Nikumbuke Lyrics

Nilipo waza kuomba
Kazikumbuka dhambi zangu
Zikanipa mashaka huenda hutojibu
Ombeni na mtapewa
Moyoni ukanikumbusha
Nikapata nguvu za kusujudu tena
Nikaanza kwa kuomba
Unisamehe dhambi zangu
Msamaha sasa wa Baba na mtoto
Nikakumbuka nakuita Baba, nikawaza je kuna Baba
Anae weza sikia sauti ya mwanae wala asijali
Moyoni nikawaza si rahisi, utelekeze ombi langu
Kama ni hivyo ombi langu leo
Bwana mi naomba kukumbukwa
Nikumbuke, nikumbuke Yesu wangu (nami nikumbuke)
Nisisahaulike kwa mazuri na wema wako (bwana nikumbuke)
Unikumbuke na uyabebe magumu yangu (nami nikumbuke)
Mi sikujua kumbe vita ni kubwa hivi (bwana nikumbuke)
Unikumbuke ugawapo Baraka zako (nami nikumbuke)
Nisisahaulike niwe mtu kati ya watu (bwana nikumbuke)
Unikumbuke unapo ratibu mambo (nami nikumbuke)
Yalipo mazuri bwana uweke na tiki zangu (bwana nikumbuke)
Umenifurahisha mungu, kwa hapa mimi nimefika
Nakiri umenikumbuka
Ni wewe huyu umefanya
Matendo yako haya mungu
Hayana mwisho kusimuliwa
Nakushukuru mungu Baba
Milele nitakutukuza
Wanifurahisha zaidi
Ukisha sema umesema
Ni nani alojuu yako, na kama yupo na aseme
Kama bahari tumevuka
Iweje mito na milima
Hakuna kama wewe mungu na hasa ukinikumbuka
Nikumbuke, nikumbuke Yesu wangu (nami nikumbuke)
Nisisahaulike kwa mazuri na wema wako (bwana nikumbuke)
Nikumbuke na uyabebe magumu yangu (nami nikumbuke)
Mi sikujua kumbe vita ni kubwa hivi (bwana nikumbuke)
Unikumbuke ugawapo Baraka zako (nami nikumbuke)
Nisisahaulike niwe mtu kati ya watu (bwana nikumbuke)
Unikumbuke unapo ratibu mambo (nami nikumbuke)
Yalipo mazuri bwana uweke na tiki zangu (bwana nikumbuke)
WATCH VIDEO
ABOUT THIS SONG
Release Year : 2022
Album : Niku Mbuke (Album)
Added By : Farida
SEE ALSO
AUTHOR
JAPHET ZABRON
Tanzania
Japhet Zabron is a gospel artist, singer, gospel songwriter and a guitarist from Tanzania a mem ...
YOU MAY ALSO LIKE