Home Search Countries Albums

Hakuna Kama Wewe Mungu

CHRIS MWAHANGILA

Hakuna Kama Wewe Mungu Lyrics

Petro na Yohana walikuwa wakikwea
Majira ya saa tisa kwenda hekeluni kusali
Petro na Yohana walikuwa wakikwea
Majira ya saa tisa kwenda hekeluni kusali

Katika mlango uitwao mzuri
Palikuwa na kiwete tangu kuzaliwa hajatembea
Katika mlango uitwao mzuri
Palikuwa na kiwete tangu kuzaliwa hajatembea

Alipowaona akataraji kupata kitu kwao
Alipowaona akataraji kupata sadaka kwao
Wakamwambia hatuna fedha wala dhahabu
Ila hiki tukupacho ndicho tulicho nacho

Kwa jina la Yesu simama uende
Kwa jina la Yesu simama uende

Ghafla akawa mzima akaanza kutembea
Akarukaruka sana akimtukuza Mungu wao
Ghafla akawa mzima akaanza kutembea
Akaingia hekaluni akimsifu Mungu wa mbinguni

Akisema 

Hakuna kama wewe Mungu, hakuna kama wewe
Hakuna kama wewe Yesu, hakuna kama wewe
Hakuna kama wewe Mungu, hakuna kama wewe
Hakuna kama wewe Yesu, hakuna kama wewe

Hakuna kama wewe Mungu, hakuna kama wewe
Hakuna kama wewe Yesu, hakuna kama wewe

Alipoingia hekaluni watu wakamtambua
Aliporukaruka sana watu wakamtambua
Huyu si ni yuleyule aliyekuwa mlangoni
Huyu si ni yuleyule aliyekuwa mlemavu
Huyu si ni yuleyule aliyekuwa masikini

Kumbe Mungu akifanya jambo watu watakutambua
Mungu akikuinua kutoka chini, watakutambua
Akirejesha heshima iliyopotea watakutambua
Akishakuponya ugonjwa wako watakutambua

Akirejesha heshima iliyopotea watakutambua
Akishakubariki sana watakutambua
Akirejesha heshima iliyopotea watakutambua
Akikupaka mafuta kama Daudi watakutambua

Watamtukuza Mungu wako
Watamwinua Mungu wako
Watamsifu Mungu wa mbinguni
Watalitukuza jina lake wakisema

Hakuna kama wewe Mungu, hakuna kama wewe
Hakuna kama wewe Yesu, hakuna kama wewe
Hakuna kama wewe Mungu, hakuna kama wewe
Hakuna kama wewe Yesu, hakuna kama wewe

Hakuna kama wewe Mungu, hakuna kama wewe
Hakuna kama wewe Yesu, hakuna kama wewe

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG

Release Year : 2019

Album : Hakuna Kama Wewe Mungu (Single)

Copyright : (c) 2019

Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

CHRIS MWAHANGILA

Tanzania

Christopher Mwahangila is a gospel artist from Tanzania. ...

YOU MAY ALSO LIKE