Home Search Countries Albums

Koma Corona Lyrics


Korona umeleta tafarani
Hatutembeleani nyumbani
Kwa marafiki vikao vingi
Umevitawala wewe

Barabarani tuvae maski
Tuingie hapo tuoshe mkono hi
Hauitaki halaiki ya watu
Wananchi tutakula nini?

TV, gazeti, redio nchini
We Corona utaisha lini?
Hauitaki halaiki ya watu
Wananchi tutakula nini?

Ooh dunia mzima mtaani o
Taarifa nyingine hakuna o
Ni yako ni yako ee
Ni yako Corona

Madakitari kimbilio letu
Unawamaliza wewe sasa
Nimechoka sekeseke zako, mie 
Zimechosha masikio koma

Koma Corona wewe koma
Unatumaliza we koma
Corona wewe koma
Utaisha lini koma

Corona wewe koma
Unatumaliza we koma
Corona wewe koma
Utaisha lini ayee

Eeh una nguvu za ajabu 
Napata taabu
Nakosa usingizi hey
Unanifanya mapema nilale 
Na nnje nisitoke

Niambie nikupe siku ngapi
Ujisalimishe duniani wewe
Kama ni mwaka hatutaki
Utausambaratisha ulimwengu wote

Ona na vifo vyako vinahesabu
Unao waadhiri hawana matibabu
Wanapata taabu
Kisa Corona wewe

Ooh dunia mzima mtaani o
Taarifa nyingine hakuna o
Ni yako ni yako ee
Ni yako Corona

Madakitari kimbilio letu
Unawamaliza wewe sasa
Nimechoka sekeseke zako, mie 
Zimechosha masikio koma

Koma Corona wewe koma
Unatumaliza we koma
Corona wewe koma
Utaisha lini koma

Corona wewe koma
Unatumaliza we koma
Corona wewe koma
Utaisha lini ayee

Mola tuepushie 
Na hili janga la korona
Tushushie na neema zako
Mola 

Corona eeh, Corona ooh
Corona kilio Corona
Corona aah, Corona

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2020


Album : Koma Corona


Copyright : (c) 2020


Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

CHIKUZEE

Kenya

Chikuzee is an artist from Kenya. ...

YOU MAY ALSO LIKE