Home Search Countries Albums

Kipofu

BEST NASO

Kipofu Lyrics


Hivi unajua Mungu ameumba dunia
Na yaliyomo yote
Na ametuambia tuwapende na kuwaheshimu
Wanawake wote

Basi muda ulivyotimia
Nami nikatafuta mpenzi wa kuishi naye
Na ndo hapa nikaamini dunia ina maajabu yake
Mpenzi wangu akaumwa, yakawa mekundu macho yake

Huku na huku hospitali
Macho yamekoma kuona
Mke wangu kawa kipofu
Walimwengu wanataka nimwache

Ingawa wanakuita kipofu
Mie nakupenda kwako natulianga
Ingawa wanakuita kipofu
Mie nakupenda kwako natulianga

Aah, natulia
Nife unizike nikuzike
Aah, natulia
Wanayoyasema usiogope
Aah, natulia
Nitakuchagua leo kesho hata na milele
Aah, natulia
Mwingine sina, sina kama wewe

Ukishindwa kutembea usipate taabu
Nitakubeba mgongoni
Hata chakula siwezi nile
My love mpaka ule wewe

Na ukilala lazima nikuombee
Nikukinge na magonjwa ulale salama
Nami binadamu nimeumbwa
Ndo maana siwezi ringa

Kesho yangu aijua muumba
Matokeo Yanga na Simba

Siwezi sema eti nikuache
Kisa ukipofu nitamkufuru Mungu
Njoo njoo mama anaita
Kama umechoka kifuani sinzia
Hallo napiga guitar
Wimbo mzuri kwa ajili yako

Ingawa wanakuita kipofu
Mie nakupenda kwako natulianga
Ingawa wanakuita kipofu
Mie nakupenda kwako natulianga

Aah, natulia
Nife unizike nikuzike
Aah, natulia
Wanayoyasema usiogope
Aah, natulia
Nitakuchagua leo kesho hata na milele
Aah, natulia
Mwingine sina, sina kama wewe

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2020


Album : Kipofu (Single)


Copyright : (c) 2020


Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

BEST NASO

Tanzania

Best Nasso is an artist/songwriter  from Tanzania. ...

YOU MAY ALSO LIKE