Sabuni ya Roho Lyrics
Wanasema kwenye dunia
Ukiwa na pesa shida
Wanasema kwenye dunia
Ukiwa na pesa utang'aa
Unaweza fanya lolote
Ukatukana yoyote
Na watu wakasema sawa
Unaweza fanya chochote
Na ukampiga yoyote
Na bado wakasema sawa
Yarabi tustahi
Wake za watu wanasaliti ndoa
Kwa sababu ya pesa
Yarabi tustahi
Ona maskini wanakosa haki
Kwa sababu ya pesa
Miziki tena kanisani wanaiuza dini
Kwa sababu yake pesa
Kwa zaidi ata niliyempenda naye
Amenisaliti
Anasema kachoshwa na shida
Na hivi karibuni anaolewa
Oooh mpenzi ndoa oooh
Sina changu naumia
Oooh pesa, pesa sabuni ya roho
Pesa, pesa sabuni ya roho
Oooh pesa, pesa sabuni ya roho
Pesa, pesa sabuni ya roho
Namuona babu mzee
Anatumikishwa kazi na kijana mdogo
Namuona bibi mzee
Anabebeshwa mizigo na vijana wadogo
Naziona nchi zinapigana
Watu wanarogana eeeh
Kwa sababu ya pesa
Namuona mama anatukanwa
Tena na katoto kadogo
Kwa sababu ya pesa
Mtaani kwetu kuna wazee
Wameoa vibibi vidogo
Kwa sababu ya pesa
VH wadogo wanazaa
Hakuna anayekataa
Kila kona za mitaa
Machokoraa wamezagaa
Ona wanaishi vizuri
Wale wenye pesa zao
Magari yao mazuri
Wale wenye pesa zao
Tena wanavaa vizuri
Wale wenye pesa zao
Pesa kiboko kiboko ya njaa
Oooh pesa, pesa sabuni ya roho
Pesa, pesa sabuni ya roho
Oooh pesa, pesa sabuni ya roho
Pesa, pesa sabuni ya roho
Kama pesa zingekuwepo
Unadhani angekuwepo?
Au zingekuwepo pesa
Haya yote yangekuwepo?
Hili swali jibu swali
Usiniulize maswali
Kichwa changu kinauma
Nabaki natafakari
Kama pesa zingekuwepo
Unadhani angekuwepo?
Au zingekuwepo pesa
Haya yote yangekuwepo?
Hili swali jibu swali
Usiniulize maswali
Kichwa changu kinauma
Nabaki natafakari
WATCH VIDEO
ABOUT THIS SONG
Release Year : 2019
Album : Sabuni ya Roho (Single)
Copyright : (c) 2019
Added By : Huntyr Kelx
SEE ALSO
AUTHOR
YOU MAY ALSO LIKE