Home Search Countries Albums

Nayumba

WYSE

Nayumba Lyrics


Sasa ni mchana jua kali
Ila naona giza
Hata nikiwasha kandili
Mi sipati mwangaza

Natafuta afadhali
Wa kujiegemeza
Wengi walionijali 
Nimewapoteza

Hivi visiki vya kila leo
Vizuri naona kwenye video
Nawaza lini nitapanda cheo
Ila natoka kapa

Hata marafiki nilosoma nao
Na marafiki nilosoma nao
Wote sasa mi si mwenzao
Yaani wameniacha

Kusema maisha yamenikatili
Hadi nachoka mi kusubiri
Si mraba si mstatili
Sina shufa wala  mitili

Nayumba, nayumba
Kama kosa linasali
Nayumba nayumba
Ila bado majabali

Nayumba nayumba
Shida zinanikabili
Nayumba nayumba
Wala sioni afadhali

Baba mwenye nyumba kisirani
Nimezongwa na madeni
Mazonge purukushani 
Balaa juu ya balaa

Hata mpenzi nyumbani
Anavumilia mengi
Isije mtoka imani
Akaja ikata tamaa

Nishasota kwenye magazeti
Kushinda mikeka kubeti
Chawa nilishindwa kufeki
Cha mtu kushika siwezi

Nishazungukaga na vyeti
Nikawekwa sana mtu kati
Nishapiga dumba sina bali 
Mi na keeper nikakosa penalti

Kusema maisha yamenikatili
Hadi nachoka mi kusubiri
Si mraba si mstatili
Sina shufa wala  mitili

Kusema maisha yamenikatili
Hadi nachoka mi kusubiri
Si mraba si mstatili
Sina shufa wala  mitili

Nayumba, nayumba
Kama kosa linasali
Nayumba nayumba
Ila bado majabali

Nayumba nayumba
Shida zinanikabili
Nayumba nayumba
Wala sioni afadhali

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2021


Album : Nayumba (Single)


Copyright : (c) 2021


Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

WYSE

Tanzania

Wyse is a singer/songwriter from Tanzania. ...

YOU MAY ALSO LIKE