Home Search Countries Albums

Bado Lyrics


Niiii, niiini, niii?
Niiii, niiini, niii?
Je nataka kuwa na nini?
Nauliza mnataka kuwa na nini?
Wasomi mnataka kuwa na nini?
Kanisa linataka kuwa na nini?
Ndipo mjue yametimia

Dunia hey, kama kulemewa
Imelema sana 
Dunia hey, kama kuanguka
Imeanguka sana 

Hivi mnataka kuwa na nini?
Ndipo mjue yametimia 
Dunia inataka kuwa na nini?
Ndipo mjue Mungu anasema

Ona akili za wenye akili
Zimefika kikomo jamani
Maarifa ya wenye akili
Yameshindwa kabisa
Hekima ya wenye hekima haisaidii kitu

Hivi mnataka kuwa na nini?
Nauliza mnataka muone nini?
Ndivyo mjue Mungu anasema

Bado, bado, bado bado bado
Kama ni mapito, bado bado 
Kama ni magonjwa, bado bado 
Kama timbwili timbwili, bado na bado 
Kama ni heka heka, bado bado 
Msishangazwe na ya leo, bado bado 

Baragumu ya kwanza imekwisha kupigwa
Dunia ijipange 
Baragumu ya kwanza imekwisha kulia
Kanisa lijipange 
Na hapa ndipo penye imani na subira
Ya watakatifu wajipange 
Wenye masikio na wasikie neno hili
Roho asema mjipange
Na bado, bado, bado ni ishara tu

Basi inueni macho yenu
Tazama vilele vimeinama
Wafalme wamechanganyikiwa
Wenye akili hawana la kufanya
Manabii maono yamekoma
Ufunuo maono yamekoma
Ayaa sasa dunia yote mikono juu
Semeni Mungu pekee ndiye Bwana 

Basi inueni macho yenu
Tazama vilele vimeinama
Wafalme wamechanganyikiwa
Wenye akili hawana la kufanya
Manabii maono yamekoma
Ufunuo maono yamekoma, bado

Nani basi asimame, mbele za Mungu aseme
Alete moja nyingine ashindane na Mungu tuone

Maneno ya Mungu kamwe hayatapita
Nasema mjipange
Kengele ya hatari imeshakwisha kulia
Nasema mjipange
Bado, bado, bado ni ishara tu

Bado, bado, bado bado bado
Na magonjwa bado, bado bado bado 
Na shida bado, bado bado bado
Njaa na matetemeko, bado bado bado
Msishangazwe na ya leo, bado bado bado
Msisitishwe na ya leo, bado bado bado
Ah nasema bado, bado bado bado
Uwiii, bado bado bado

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2021


Album : Miamba Imepasuka (Album)


Copyright : (c) 2021


Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

ROSE MUHANDO

Tanzania

Rose Muhando is an award winning Gospel Singer from Tanzania. ...

YOU MAY ALSO LIKE