Ex Boyfriend Lyrics
Leo nakula kwa macho
Nguvu ya kusema sina
Maneno ya mipasho
Na jeuri vimeshazima
Nilishafuta namba zako
Nikachoma picha zako
Sikujali ulivyolia
Mbele ya mashoga zako
Nikasema uende zako
Nguo nikakutupia
Na zaidi uliuguza vidonda
Kwa vipigo manyanyaso kila siku
Kwa mawazo ukakonda
Niko bizy kucheat
Na fungwa zilinibembeleza, nikakubeza
Unanuka nani kakutelekeza
Macho makengeza, miguu ya pweza
Kuwa nawe nikasema niliteleza
Leo unapendeza wamekutengeneza
Wanaume wenye mali wenye fedha
Sasa unajiweza siwezi kujikweza
Najutia nafasi kuipoteza, leo aibu yangu
Ex Boyfriend, Ex Boyfriend, Ex Boyfriend
Siitwi tena hunny baby jina langu limekuwa
Ex Boyfriend, Ex Boyfriend, Ex Boyfriend
Sikujuwa kumbe taabu pekee yangu naugua
Nawaza nilifeli wapi? kusema sikutaki
Sura ya baba na kitambi cha magasi
Sa una mtanashati vitozi tena smarti
Mtu wa gym tena ana six packi
Mi nipo juu ya bati sina mikakati
Ghetto mwendo chai na chapati
We ushahama Mburati una nyumba Masaki
Mnachoma nyama kila siku party
Ushanipiga mikuki, Aah!
Insta mi sifurukuti, Aah!
Mambo ya gauni suti, Aah!
Mkifanya photo shooti, Aah!
Mapenzi hayana commando
Mwenzako inaniuma roho
Natamani nikuite njoo
Turudi kama before
Kumbe shepu ilijificha kwenye dera
Hizo skinny jeans mama zinakera
Utaniletea kadi kwenye machela
Siku wakikuvalisha shela
Na ulinibembeleza, nikakubeza
Unanuka nani kakutelekeza
Macho makengeza, miguu ya pweza
Kuwa nawe nikasema niliteleza
Leo unapendeza wamekutengeneza
Wanaume wenye mali wenye fedha
Sasa unajiweza na sio najikweza
Najutia nafasi kuipoteza, leo aibu yangu
Ex Boyfriend, Ex Boyfriend, Ex Boyfriend
Siitwi tena hunny baby jina langu limekuwa
Ex Boyfriend, Ex Boyfriend, Ex Boyfriend
Sikujuwa kumbe taabu pekee yangu naugua
(Nusder)
WATCH VIDEO
ABOUT THIS SONG
Release Year : 2020
Album : Flowers/ Ex Boyfriend (Album)
Copyright : (c) 2020 Wasafi Records.
Added By : Huntyr Kelx
SEE ALSO
AUTHOR
RAYVANNY
Tanzania
Raymond Shaban Mwakyusa (born 22 August 1993), better known by his stage name Rayvanny, is a Tanzani ...
YOU MAY ALSO LIKE