Home Search Countries Albums

Mtoto Wa Taifa Freestyle

RAPCHA

Mtoto Wa Taifa Freestyle Lyrics


Ikawa usiku ikawa asubuhi 
Nkaivuta pumzi ya dunia nikiwa nalia aliyenibeba simjui
Sauti ya nesi ikasikika ikisema hongera 
umepata mtoto wa kiume fanya dua wasimtwae maadui

Baba alikua mkulima 
Mama alikuwa mwanaharakati mwisho akaingia kwenye siasa mazima 
Nkiwa na Dada angu mmoja kaka wawili
Tumeishi miaka yote sikuona baba akimvunjia mama heshima

Nimeonja chakula Bara Na zanzibar nzima
Mama anayajulia mapishi wallahi anafaa heshima
Baba hakuota kitambi cha Baa, madiko tu 
Na nlikua mtoto wa mwisho Basi kwa Ma nlideka tu

Siku zikaenda nkaanza kukua 
Nikagundua mama anapambania ndoto 
Iliyo kubwa mithili ya jua ikiwa tuliishi kwenye dunia
Ambayo haikumpa nafasi mwanamke so nikaona sio rahisi tusua

Mwaka 2000 mama siasa ikaanza kolea
Akawa mjumbe bunge la zenji akaanza kuongea
Kwakuwa ana sauti ya upole wanaume wakamchukulia poa
Kama utani akawa Waziri akatoboa
 
Haikuwa rahisi kama inavyodhaniwa 
Mama alijitoa kwenye siasa na familia akaipigania
Umakini ndo ulifanya safari yake iliyokua ndefu ikawa na tija
Akijaribu ndoto kuifikia

Siku zikazidi kimbia
Kaka angu mkubwa akawa mfanya biashara na akajisimamia
Dada angu wanu akafata nyayo za mama kwenye siasa akaingia
Mie mziki ukanihitaji nkawatimbia

2015 akabadili hadithi
Mama alijiingiza kwenye mchakato wa urais
Ilikua Hatua ngumu na wengine walimdiss
Waliodhaniwa kuweza walishindwa nahisi

Basi Mwisho wa siku future ikaamua
Na siku zote alipangalo Mungu watoto wadogo hawaezi pangua
Akisha sema itakua inakua
Hapo hata ubane kende vipi zaidi Sana utazipasua  

Yes Mungu akabless mambo yakatiki
Mama ndio akawa vice president wa kwanza wa kike
Nliona kama ndoto ila mchizi sikutaka niamke
Nkawa inspired vile mama ameishi na ndoto yake

Miaka mitano ikapita 
Iliyojaa vioja na visanga Jah anabless siku zikapita
Uchaguzi mkuu mama akaenda mitano tena 
Ila hata miezi haikupita

Usiku mmoja nkapigiwa simu
Rapcha bora umepokea nna ishu muhimu
kuna taarifa Nzito imenifikia
Tumempoteza Rais wa jahmuri ya muungano wa Tanzania

Taarifa kote zikafika
Vilio na taharuki ikaibuka mitandao ikaandika
Kulingana na katiba ya nchi yetu baada ya kumpoteza raisi
Kuna utaratibu ukawa unafanyika

Kwa kufata katiba Rais akifariki 
Makamu wake ataongoza muda wote uliobaki
Yakazuka maneno sa itakuaje, ngoja tuone,
Mh kweli huyu mama, acha tusubiri tuone 

Tukiwa tunaendelea na msiba
Ikafatwa Kama vile ambavyo imeandikwa kwenye katiba 
March 19 Asubuhi mama akaapishwa kuwa Rais wa Tanzania Wa Awamu ya sita

Niliona nipo ndotoni 
Mama anatembea akikagua gwaride akiwa na ushungi kichwani
Mama leo anaandika historia mpya ya kuwa rais wa kwanza mwanamke nchini

Naona Leo Mama anasimama anahutubia
Na mwiko haujawa Mzito nyumbani anatupikia
Vizinga simpigi alhamdullilah Mchele unaingia
Inspiration ya watoto wengi wa kike hii Dunia 

Siku nzuri zinakuja 
Namtazama Simba anaeongoza nchi kwa lafudhi ya unguja
Kazi iendelee karata zichangwe mchezo ushaujua 
Hatuogopi Shari Ukinizingua nakuzingua

Asante kwa Kunisikiliza
Naitwa Rapcha
Last King Of 90's Baby 

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2021


Album : Mtoto Wa Taifa Freestyle (Single)


Copyright : (c) 2021


Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

RAPCHA

Tanzania

Rapcha aka The Last King of 90’s, real name Cosmas Paul Mfoy is a young rapper from Tanza ...

YOU MAY ALSO LIKE