Home Search Countries Albums

Africa

MUU FLOW

Africa Lyrics


Natazama mito milima na mabonde
Kwa jicho la mbali mi nahusisha vile vyote
Natazama vito dhahabu na vikombe
Wote wa asili ulotanda pande zote

Jangwa la Sahara na vitu vya dhamani
Milima ya Usambara vilivyomo humo ndani
Africa ya busara ina tunzo ya kidani
Lugha safi ile sana wasopenda buriani

Viongozi mashujaa Afrika ya leo
Ushauri nasaha ndio yetu pembejeo
Mali nyingi bwana dah ukoloni mambo leo
Silabasi za mitaa makabila za cheo

Pembejeo na kilimo watu wa Africa
Bahari ya Hindi imependeza, Africa
Mito na milima inavutia, Africa
Africa ya Nyerere na Mugabe
Nelson Mandela Tanzania na Zibambwe

Unanidai zawadi, zawadi yangu mapenzi
Mapenzi yangu ya dhati 
Mi nakupa wewe Africa yangu nakupenda sana
Na najivunia wewe, najivunia wewe yeah

Wa mang'ati wamasai makabila ya siri
Hapa yero subai na mifugo ndo dili
Nabaki nitabaki Africa 
Na nikifa na nizikwe Africa
Utanda uko wazi wazi Africa
Utanda wa makazi wenye azi Africa 
Madini ya pekee Tanzania, Tanzanite
Tubengwa sherehe hivi vitu alright

Mungu Baba umebariki Africa nzima
Twaishi kwa amani na kupendana
Umetupa mnyama tele wa kila aina 
Ukatupa lugha tele zisizofanana

Unanidai zawadi, zawadi yangu mapenzi
Mapenzi yangu ya dhati 
Mi nakupa wewe Africa yangu nakupenda sana
Na najivunia wewe, najivunia wewe yeah

Najivunia kuwa uzao wa tumbo lako Africa
Africa wewe ni mama yangu
Umenilea, umenifunza utu wewe
Mila na desturi zako zimejawa ustaarabu Africa
Africa aah, Africa yeah oooh, yelelele lele

Unanidai zawadi, zawadi yangu mapenzi
Mapenzi yangu ya dhati 
Mi nakupa wewe Africa yangu nakupenda sana
Na najivunia wewe, najivunia wewe yeah

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2020


Album : Africa (Single)


Copyright : (c) 2020


Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

MUU FLOW

Tanzania

Muu Flow also known as Young King is a singer, songwriter and a rapper from Tanzania. Muu Flow ...

YOU MAY ALSO LIKE