Home Search Countries Albums

Nyumba Kubwa

MENINA

Nyumba Kubwa Lyrics


Kwani vipi unanidai
Unajifia mwizi wangu
Hadi kikombe cha chai
Unasera kwa mume wangu

Mwenzako nalala naye naamka naye
Mipango napanga naye yeye
Nguza zako kelele unaongopewa we
Vitimbi vyako ni bure eeeh

Kabla hujajitambulisha
Tayari nimeshakujua
Simu unajipigisha mwezako unatusumbua
Usiku wa manane, mwenzako unachumba ndimu
Punguza sebene unatakata steam

We nyumba ndogo wee, nimemshona mdomo
Ndio maana haongei tena, nimemshona mdomo
We nyumba ndogo wee, nimemshona mdomo
Anajiibia amekwama, nimemshona mdomo

Kama anakupenda kweli
Asingerudi kwnagu usiku nilale nayeye
Nimezipata habari 
Analitaja jina langu akiwa ndani na wewe

Mikapu za bukubuku, zitakukausha sura
Suku miguu ya kuku, bwana hilo lamkera
Nampa  misoso moro, sambusa za nyama
Urojo wa babu choro, ndo maana kakwama
We unamlisha viporo ubwebwe wa jana
Matunzo yako doro bibiye umekondeana

Usiku wa manane, mwenzako unachumba ndimu
Punguza sebene unatakata steam

We nyumba ndogo wee, nimemshona mdomo
Ndio maana haongei tena, nimemshona mdomo
We nyumba ndogo wee, nimemshona mdomo
Anajiibia amekwama, nimemshona mdomo

Pombe hanunui kitonga anapenda
Jeuri hajui baraka ya madanga
Bughira mbughira kaa pembeni, ooh mama
Bughira mbughira kaa pembeni, huna jipya bwana
Bughira mbughira kaa pembeni, nyumba zimeshindikana

Wale watakula leo
Wa kesho watajua mwenyewe
Menina hapa bi Mkubwa 

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2021


Album : Nyumba Kubwa (Single)


Copyright : (c) 2021


Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

MENINA

Tanzania

Menina Legria is an artist from Tanzania. ...

YOU MAY ALSO LIKE