Home Search Countries Albums

Mbona

MATTAN

Mbona Lyrics


Mimi sitaki tena kusikia umeniumiza
Alpha na Omega mwanzo mwisho katu sitokuwaza
Umenisulubu kwa adhabu
Nami mdhaifu kwako nyang'afu

Na si unajua tu wewe
Mwenzako maumivu kiwewe
Yaani umetenda tu wewe 
Kifaranga manjonzi furaha ya mwewe

Si unajua tu wewe
Mwenzako maumivu kiwewe
Yaani umetenda tu wewe 
Oooh 

Na mbona mbona mbona mbona?
Upendo daraja limevunjika
Mbona mbona mbona mbona?
Furaha umebadili kuwa maumivu

Mbona mbona mbona mbona?
Nafanyaje ndo hivi najikokota
Mbona mbona mbona mbona?
Kiranga mbele nimebaki bubu

Lahili wa nahari
Silali unono zake hiana
Akaenda upepo mwanana
Kavuka nyika nami simanzi

Sipati jawabu juu ya hili
Jambo najiuliza
Umefichuka kichaka uloficha mechacha
Niparua makucha mmmh
Kutaka kunikomoa
Nia yako kusudi umevuja pakacha 

Na si unajua tu wewe
Mwenzako maumivu kiwewe
Yaani umetenda tu wewe 
Kifaranga manjonzi furaha ya mwewe

Si unajua tu wewe
Mwenzako maumivu kiwewe
Yaani umetenda tu wewe 
Oooh 

Na mbona mbona mbona mbona?
Upendo daraja limevunjika
Mbona mbona mbona mbona?
Furaha umebadili kuwa maumivu

Mbona mbona mbona mbona?
Nafanyaje ndo hivi najikokota
Mbona mbona mbona mbona?
Kiranga mbele nimebaki bubu

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2020


Album : Mbona (Single)


Copyright : (c) 2020


Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

MATTAN

Tanzania

Mattan is an artist from Tanzania. ...

YOU MAY ALSO LIKE