Aku Lyrics

Vipi nitaziba pancha
Maana moyo ushatoboka
Kisimani bila ngaka
Mbebaji nikachoka
Nahisi uchuro ama mizimu
Nimepinga dua zangu
Mizani pima kilo
Na ni doctor wa kutibu maradhi yangu
Basi moyo tulia kinywa kikose maneno
Mengi nishayafumbia japo sheria msumeno
Basi moyo tulia kinywa kikose maneno
Mengi nishayafumbia japo sheria msumeno
Aku sitaki tena
Aku kuugua maradhi na tiba hakuna
Aku sitaki tena
Aku kuugua maradhi na tiba hakunaga
Uwezo wangu wa taratatili mapungufu ya nyota
Kichwa mawazo maradhi ya mwili dah yaani nachoka
Kanitia doa kwenye ndoano kanivua vua
Najishongondoa kwenye mabano naungua jua
Ndege kisirisiri nimenaswa kisa mpunga
Japo nisaidie penzi langu nyota ya ponda
Basi moyo tulia kinywa kikose maneno
Mengi nishayafumbia japo sheria msumeno
Basi moyo tulia kinywa kikose maneno
Mengi nishayafumbia japo sheria msumeno
Aku sitaki tena
Aku kuugua maradhi na tiba hakuna
Aku sitaki tena
Aku kuugua maradhi na tiba hakunaga
Tiba hakunaga
Kibaku baku, nachafukwa na nyongo
Kibaku baku, mwili umekufa nganzi
Kibaku baku, nitavumilia japo kishingu upande
Kibaku baku, nachafukwa na nyongo
Kibaku baku, japo kishingu upande
Kibaku baku, nitavumilia na nitazoea
WATCH VIDEO
ABOUT THIS SONG
Release Year : 2020
Album : Aku (Single)
Copyright : (c) 2021
Added By : Huntyr Kelx
SEE ALSO
AUTHOR
YOU MAY ALSO LIKE