Baki na Mimi Lyrics

Kukutazama ukitabasamu
Nika kuwatch movie za Afro
Siwezi boeaka
We ndo kitabu mi ndo kalamu
Niliumbwa kwa ajili yako
Kama masai na rubeka
Ninatamani ningewa yako mavazi
Ungewa si ua ama kasupu ka mbaazi
Ningewa sembe mukimo ama chapati
Baki na mimi, na mimi
Kipenzi, kipenzi
Nikushughulikie aah
Kila asubuhi, nirauke ili nikupikie
Nikuogeshe, ogeshe
Nikuvishe, vishe
Mpaka uvutie aah
Kamba za viatu beiby, mi nikufungie
Baki na mimi
Nitang'ang'ana nikue chochote ambacho unatamani
Oooh baki na mimi
Nitakonda utavimba, utakopa nitalipa mama
Baki na mimi
Naapa kukutunza kuliko wako wa zamani
Oooh baki na mimi
Ukisota nitaiba, utapona na tiba mama
Baki na mimi!
Na kama ungewa, mwanasiasa
Ningepiga campaign zako
Nikusifie, kwa giza na mwangaza
Mpaka kwa maadui zako mmmh
Nitakubusu bila uoga hadharani
Ili wajue wewe ndo wangu mwandani
Ningewa kijiko lazma ungewa sahani
Kututenganisha hilo haliwezekani
Baki na mimi, na mimi
Kipenzi, kipenzi
Nikushughulikie aah
Kila asubuhi, nirauke ili nikupikie
Nikuogeshe, ogeshe
Nikuvishe, vishe
Mpaka uvutie aah
Na ukichoka nikubebe, wivu wasikie
Baki na mimi
Nitang'ang'ana nikue chochote ambacho unatamani
Oooh baki na mimi
Nitakonda utavimba, utakopa nitalipa mama
Baki na mimi
Naapa kukutunza kuliko wako wa zamani
Oooh baki na mimi
Ukisota nitaiba, utapona na tiba mama
Baki na mimi!
WATCH VIDEO
ABOUT THIS SONG
Release Year : 2020
Album : Baki na Mimi (Single)
Copyright : (c) 2020
Added By : Huntyr Kelx
SEE ALSO
AUTHOR
LETEIPA THE KING
Kenya
Vampk254 also known as Leteipa the King is an Afro pop music artist from Kenya. ...
YOU MAY ALSO LIKE