Home Search Countries Albums

Amelipa Deni Yangu

LAVENDER OBUYA

Amelipa Deni Yangu Lyrics


Baruch Adonai ewe Mungu Baba
Baruch Adonai Mungu wa baraka
Baruch Adonai Mungu wa agano

Uliyonitendea sitaweza sahau
Uliyonitendea nitasimulia mataifa
Mwanadamu hajui jinsi unavyonidhamini
Baba ulinipenda kabla sijakujua wewe

Ukamtoa mwanawe Yesu awe kafara
Bwana Yesu ukachinjwa ili mimi niishi
Upendo wako kwetu mimi sitaweza sahau
Upendo wako Baba umezidi ule wa mama

Baruch Adonai, eeh Baruch Adonai
Wewe ni Mungu
Baba umelipa

Umelipa deni yangu baba umelipa
Deni ya laana zangu
Umelipa deni yangu baba umelipa
Deni ya mateso
Umelipa deni yangu baba umelipa

Yesu wa Masia
Yesu wa Masia
Yesu wa Masia

Mimi nina sababu ya kukusifu ee Bwana
Mimi nina sababu ya kukusifu aah Masia
Kila ulimi ukiri kwamba Yesu ni Bwana
Kila goti na lipigwe mbele zako Masia

Katikati ya wezi ulikufa kwa niaba yetu
Deni ye Edeni we baba ulibeba kwa ajili yetu
Kifo cha aibu ukafa, ulikufa kwa ajili yetu
Tulifaa kudharauliwa, uliteswa kwa ajili yetu
Tulifaa kutwmwa mate ulitendwa kwa ajili yetu

Ah masia ooh
Yesu wa Adonai wewe ni Mungu
Yesu umelipa Baba

Umelipa deni yangu baba umelipa
Kweli umelipa Yesu
Umelipa deni yangu baba umelipa
Deni ya makosa yangu
Umelipa deni yangu baba umelipa
Deni ya mizigo yote
Umelipa deni yangu baba umelipa
Uliyetundikwa pale Calvary
Umelipa deni yangu baba umelipa
Baba wewe ulisema yote yamekwisha
Umelipa deni yangu baba umelipa
Mimi kamwe sidaiwi tena
Umelipa deni yangu baba umelipa
Gharama ya mauti
Umelipa deni yangu baba umelipa
Gharama ya dhambi zangu zote
Umelipa deni yangu baba umelipa
Wewe umelipa wewe Bwana
Umelipa deni yangu baba umelipa
Yesu amelipa yote
Umelipa deni yangu baba umelipa
Yesu amelipa yote
Umelipa deni yangu baba umelipa
Amelipa Yesu, Amelipa Baba

 

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2020


Album : Amelipa Deni Yangu (Single)


Copyright : (c) 2020


Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

LAVENDER OBUYA

Kenya

Lavender Obuya is a gospel artist from Kenya. ...

YOU MAY ALSO LIKE