Home Search Countries Albums

Nikomeshe

LAVA LAVA

Read en Translation

Nikomeshe Lyrics

Nimekuweka wallpaper 
Tangu tumeachana
Video zote nimeziweka 
Kumbukumbu tukidekezana

Mmmh baadhi ya picha nimehifadhi
Kwa laptop simu ikileta shida (Shida shida)
Ka memory kenye hakana virus
Na wezi nao wasije wakaiba (Iba iba)

Nilisema nisikunfollow Insta wala kukublock
Kumbe nafanya kazi ya kanisa, presha najipa stroke
Ili si utabadilika kumbe fikra zangu potofu
Nampa kiziwi speaker, kioo nampa kipofu

Wewe unaenjoy ninabaki mjinga ndemwa
Kisa kwako sikohoi ndo kila siku masinema
Au kisu sinoi sijui kulenga mi nadema 
Nitoe na roho basi uenjoy nifike unizike tu mapema

Nikomeshe, malipo duniani yote ni mapito
Nikomeshe, kila lenye mwanzo halikosi mwisho
Nikomeshe, jua kila mtihani una suluhisho
Nikomeshe, we nione hamnazo fungu langu lipo

Mmmh kinachoniumiza yeye ndo yangu dawa
Akinitibu napona
Ona kanimimina sanitizer kaninawa
Utadhani Corona

Moyo wangu kwake niliugawa 
Nikampa yeye mbona
Kapeperuka kama ana mabawa
Kaniacha nasonona 

Sonona sono, penzi kalikatisha njiani
Sonona sono, mwambieni japo awe na imani
Sonona sono, mi mwenzake nitapendwa na nani?
Sonona sono, iiii....

Nilikuwa sijajua kuna binadamu na watu
Kumbe nawe ulikuwa nusu kenge nusu chatu
Unaniumiza ingali wajua ndo unayenitosha kiatu
Nenda nitasoma dua nitakaa hata hiatu

Nilisema nisikunfollow Insta wala kukublock
Kumbe nafanya kazi ya kanisa, presha najipa stroke
Ili si utabadilika kumbe fikra zangu potofu
Nampa kiziwi speaker, kioo nampa kipofu

Wewe unaenjoy ninabaki mjinga ndemwa
Kisa kwako sikohoi ndo kila siku masinema
Au kisu sinoi sijui kulenga mi nadema 
Nitoe na roho basi uenjoy nifike unizike tu mapema

Nikomeshe, malipo duniani yote ni mapito
Nikomeshe, kila lenye mwanzo halikosi mwisho
Nikomeshe, jua kila mtihani una suluhisho
Nikomeshe, we nione hamnazo fungu langu lipo

Nitajiliwaza, mwenyewe nitajiliwaza
Nitajiliwaza, nikilia nitanyamaza
Nitajiliwaza, mwenyewe nitajiliwaza
Nitajiliwaza, nikilia nitanyamaza

Nikilia lia...

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG

Release Year : 2021

Album : Nikomeshe (Single)

Copyright : (c) WCB Wasafi.

Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

LAVA LAVA

Tanzania

Lava Lava is a Tanzanian musician signed under Wasafi WCB Record label. ...

YOU MAY ALSO LIKE