Home Search Countries Albums

Bado Lyrics


(Sultan 001)
Zile issue na kuimba imba
Kwote maredio na runinga
Nikaonekana kuwa bingwa
Ila wapi bado

Nikashauriwa kwenda Pemba
Umezima moto kwneye kinga
Yote kwa kufunga na kuomba
Ila wapi bado mmmh

Maneno ya kukatisha tamaa
Kote navuma ila nalala njaa
Kasuku alotumwa na Jah
Leo yuko wapi amwokoe superstar

Wapo walonishika mkono Governer Joho
Kakangu kipenzi Gas na Susumila
Maneno na minong'onono kazeni roho
Msijali kwenye mziki kuna madhila

Na na najua
Alonitoa kwenye zege atanipandisha ndege
Maisha ni hatua
Jao leo segemnege ila Mungu nibebe

Mi natuma barua kwa ndugu zangu
Walodhani ndo tayari nimetoboa
Bado zinanirarua shida zangu
Maisha kwenye safari sio poa

Bado ningali natembea
Bado sijachoka naelekea mimi
Bado polepole nachechemea
Bado wowowowo uwooo

Bado ningali natembea
Bado sijachoka naelekea mimi
Bado polepole nachechemea
Bado wowowowo uwooo

[Kaa La Moto]
Ata session nimepata man ile Kimungu Mungu
Bado lipi bado kavu yaani kiuchungu chungu
Labda ni gundu au kisa labda ni ngumu
Labda humu napopita sipatii majukumu

Mnaokuza talanta mko wapi ama ndio stori ya kujuana
Au naandika sana au mnataka nisiwaimbie vya maana
Kuroga nimeshindwa, mziki na dumba una laana
Au nifanye kiki ndio niweze kujulikana

Hapana lowa tu malichele ya kurudi
Shoka halijakata gogo japo nimetumia juhudi
Saa zingine inaniishia mpaka moodi
Nishafikiria kuiacha ili niende kuitafuta kazi

Sikutaka kuamini kuskika hadi jiji kuu
Mambo na connection na promotion ziko juu
Hivi mpaka lini tunakosa waekezaji
Na kulala njaa na kutofaidika na hichi kipaji

Wingi wa masikitiko
Omba omba kwetu sisi ni mwiko
Aiyee Abu asahau kiko
Ndo katoto kapate kasisimuko

Hivi ama kweli KO akili timamu
Unakwazika moyo unatabasamu
Japo ridhiki napata vyaja kwa zamu
Ila kile kikulacho ndugu adamu

Kukatwa katwa mapanga kufungwa nyororo
Ila yote naridhia
Sioni dalili za mwanga ila giza totoro
Asubuhi imekaribia

Mi natuma barua kwa ndugu zangu
Walodhani ndo tayari nimetoboa
Bado zinanirarua shida zangu
Maisha kwenye safari sio poa

Bado ningali natembea
Bado sijachoka naelekea mimi
Bado polepole nachechemea
Bado wowowowo uwooo

Bado ningali natembea
Bado sijachoka naelekea mimi
Bado polepole nachechemea
Bado wowowowo uwooo

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2020


Album : Bado (Single)


Copyright : (c) 2021


Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

KO KENYA

Kenya

KO Kenya (Knock Out)  is a  Performing Artist | Songwriter | Recording artist from Kenya. ...

YOU MAY ALSO LIKE