Chekecha Lyrics
King Bibo ft Bright - Chekecha lyrics
Wanaona tunafanikiwa hawajui tunaanzaje
Wanachukia wasichojua tumepataje
Hawakuwepo mwanzao watatujuaje
Nakupenda kukuwacha sijui itakuwaje
Wanaitamani siku tukijifungia ndani
Waone tunaicheza michezo gani
Inawakera wanaisaka tafrani
Watuzushie tutibuane kama ngomani
Nikijituma kutoa hali yenye kutia huruma
Wanaleta hujuma kilio chao hawanioni
Nikirudi nyuma watasubiri sana
Ndio kwanza naunguruma
Fumba macho fumba sikio
Maneno yao usisikie
Moyo wako ufanye chojio
Sumu zao zisikuingie
Pumba chekecha, tuwe chekecha
Chekecha chekecha
Maneno chekecha, sumu chekecha
Wanadhania penzi letu bahati yandondokea
Wamepotea na kwetu hawana sera
Tunapepea tukapo yetu bendera
Na Wakituchukia tunacheza wantarambera
Tunafurahi, tunajidai
Hata siku tunazo shindia chai
Wanaona hatung'ai pesa haijai
Ndo wanavyopenda maisha yatutoe nishai
Tabasamu lako lina niongezea motisha
Nisizubae nizidi kuyafanikisha
Nahakikisha kukupenda na kukuridhisha
Wanaona pcicha tunavyo yatoboa maisha
Fumba macho fumba sikio
Maneno yao usisikie
Moyo wako ufanye chojio
Sumu zao zisikuingie
Pumba chekecha, tuwe chekecha
Chekecha chekecha
Maneno chekecha, sumu chekecha
Basi nipe mapenzi, mmmh aah mmh aah
Oooh aaah, oooh aah
Nizidishie mapenzi, mmmh aah mmh aah
Oooh aaah, oooh aah
WATCH VIDEO
ABOUT THIS SONG
Release Year : 2020
Album : Chekecha (Single)
Copyright : (c) 2020
Added By : Huntyr Kelx
SEE ALSO
AUTHOR
YOU MAY ALSO LIKE