Home Search Countries Albums

Wosia

KALA JEREMIAH Feat. ONE SIX

Wosia Lyrics

Wanangu sogeeni
Wanangu nina jambo nalotaka waambieni
Muda wangu umetimu wa kuondoka duniani
Nawaachia usia wanangu kapendaneni

Nasisitiza tena wanangu kapendaneni
Ilindeni amani kesheni mkisali
Shetani asiwarubuni fungueni macho yenu
Ili muone ya ndani

Hakika nimetenda Mungu aliyonituma
Nawaombea kwa baba msijekurudi nyuma
Mshikamano wenu gurudumu kusukuma
Msiyumbishe mashua upepo unapovuma

Wosia wako baba unanichoma sana mpaka moyoni
Yale matendo yako nitaishi nayo kwangu rohoni
Hivi kweli unaenda, kweli unaenda, kweli unaenda baba
Hivi kweli unaenda, baba unaenda, kweli unaenda baba

Sasa nazama chini macho yangu juu ya mbingu
Roho inaponyoka mbele naona ukungu
Napita katikati ya uvuli wa mauti
Moyo wangu umechoka na mwili u mahututi
Napigania nafsi na nia ni madhubuti
Naisaka pumzi yangu ya mwisho sauti

Ya malaika wa zamu inanisisitiza
Naona mwanga juu lakini chini ni giza
Mbele yangu nayaona malango ya mbinguni
Niagieni ndugu zangu tutakutana Canaani
Tazama sasa nimezungukwa na ndugu
Mikononi mwako baba naiweka roho yangu

Wosia wako baba unanichoma sana mpaka moyoni
Yale matendo yako nitaishi nayo kwangu rohoni
Hivi kweli unaenda, kweli unaenda, kweli unaenda baba
Hivi kweli unaenda, baba unaenda, kweli unaenda baba

Nimevipiga vita vilivyo vizuri
Mwendo nimeumaliza sasa nakata kauli
Shusheni mwili wangu sasa unataka kaburi
Roho yangu i tayari kwenda masafa ya mbali
Maandiko msipuuze mkajisomee Zaburi
Na nuru iwamulike kama jua la adhuhuri
Andaeni mapito watu wawanenee mazuri
Pandeni mbegu za wema mkajipatie kivuli
Ndani ya moyo wangu nimewaweka muhuri
Nitawapenda mpaka ukamilifu wa dohari
Lindeni muungano ilindeni jamhuri
Tutaonana tena ila kwa sasa kwaheri

Wosia wako baba unanichoma sana mpaka moyoni
Yale matendo yako nitaishi nayo kwangu rohoni
Hivi kweli unaenda, kweli unaenda, kweli unaenda baba
Hivi kweli unaenda, baba unaenda, kweli unaenda baba

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG

Release Year : 2021

Album : Wosia (Single)

Copyright : (c) 2021

Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

KALA JEREMIAH

Tanzania

Kala Jeremiah is an East Africa hiphop ambassador from Tanzania. ...

YOU MAY ALSO LIKE