Rafiki Lyrics
Rafiki ebu sikia huu ujio (My nigga)
Rafiki hembu anza kusonga mbio
Achana na kiki mitandao na matukio
Kwa hizi dakika chache niazime masikio
Kwa kifupi nitanena marudio
Ushayasikia kwenye televisheni na redio
Na pia nina siri mshitue na mwenzio
Maana ya kitu kizuri ule na wenzio
Rafiki nakutuma mpaka ikulu
Rafiki nakutuma kashukuru
Rafiki hebu fikisha hizi duru
Siku hizi hakuna njanja njanja kuhepa ushuru
Ndio maana nchi yangu imeanza kuwa na nuru
Kwa kifupi nakutuma magogoni
Mwambie mjomba yale tuliota ndotoni
Leo hatuamini tunayaona machoni
Ubunge wa Tazara siku hizi hakuna foleni
Wengine wanapita chini
Mwambie kakomesha wezi wa madini
Mwambie tumemwelewa watoto wa mjini
Mandege mameli muulize tutamlipa nini
Mpe pongezi kutoka mijini vijijini
Mwambie tano nyingine ni asilimia tisini
Wahujumu wamenasa kwenye chambo
Machinga wanatamba na mitambo
Fisadi amepotea kama mfuko wa Rambo
Mmewaponya mama ntilie na rungu la mgambo
Rafiki nakutuma nenda kwa uncle
Nenda Magogoni, Dodoma na Chato
Hapa ni kazi tu kazi day by day
Nenda kaseme kwa niaba ya wote
Mitaa inaimba Magufuli (Magufuli)
Vijiji vinaimba Magufuli (Magufuli)
Wanyonge wanaimba Magufuli (Magufuli)
Yaani kila kona wanaimba Magufuli (Magufuli)
Rafiki nakwamini we ni jitu la misuli
Ukifika usiogope kamhadithie vizuri
Mwambie sie wanyonge tunaimba Magufuli
Maana bila hata ada watoto wako skuli
Bodaboda zinaimba Magufuli (Magufuli)
Bajaji zinaimba Magufuli (Magufuli)
Kwanzia Tarime mpaka Mbalali
Ni lami tupu ndio maana wanga hawalali
Siku hizi hata mbungeni hawalali
Rafiki usije kufukua makaburi
Waliozikwa ndugu zetu kina Daudi Balali
Kampongeze kwa Air Tanzania
Steelglaz goji kwa hakika kapania
Standard gauge ujenzi unaendelea
Ufisadi tulioimba kukemea
Leo umenyauka kaukata kama mmea
Papi Kocha na Sea washatoka Segerea
Mwambie 2020 ameshinda kabla kugombea
Najua mengine utaongezea
Mama yangu Samia Suluhu kamsalimie na...
"Kuna msanii anaitwa Kala Jeremiah
Karibuni hivi nimemsikia ametoa wimbo
Mzuri wa kuhamasisha vijana wajitegemee
Wafanye kazi, naomba mnisalimie Kala Jeremiah
Kwa wimbo mzuri alioutoa wa kuhamasisha vijana
Ule ni uzalendo "
...na mjomba Majaliwa waambie nawaaminia
Nenda kambatize, jioni aitwe Musa
Na hao mafarao mwambie hawatamgusa
Mwambie atuvushe nchi ya ahadi ye ndo Visa
Rafiki nakutuma nenda kwa uncle
Nenda Magogoni, Dodoma na Chato
Hapa ni kazi tu kazi day by day
Nenda kaseme kwa niaba ya wote
Mitaa inaimba Magufuli (Magufuli)
Vijiji vinaimba Magufuli (Magufuli)
Wanyonge wanaimba Magufuli (Magufuli)
Yaani kila kona wanaimba Magufuli (Magufuli)
WATCH VIDEO
ABOUT THIS SONG
Release Year : 2020
Album : Rafiki (Single)
Copyright : (c) 2020
Added By : Huntyr Kelx
SEE ALSO
AUTHOR
KALA JEREMIAH
Tanzania
Kala Jeremiah is an East Africa hiphop ambassador from Tanzania. ...
YOU MAY ALSO LIKE