Zuchu Wana (Cover) Lyrics
Hunywi maji yakapita
Mi nkigunu na ushafika
Jina gani hujaniita beiby
Ushauri hutaki kabisa
Eti uniache nina visa
Vya Firauni vya Musa vingi
Nikilala naota kama unaniita
Nafumba macho, navuta shuka
Naona napumbazika
Unishikapo ndipo hapo
Nafarijika
Mambo yako, mahaba yako
Ndo maana natononoka wee
Wana wana wana wana
Pale tulipokutana
Mikono tukapeana
Macho yakatizamana
Wana wana wana wana
Pale tulipokutana
Namba kubadilishana
Nafsi kukubaliana oooh!
Nzi kidondani hufia
Wahenga walisema
Maradhi yaweza yasiwe na dawa
Kwa penzi yakapona
Rabii, amenipa nusura
Jeuri sina tena
We ndo ganzi, umenimaliza hasira
Siumwi wakisema
Nidekeze, niliwaze
Washushuke wanyamaze
Nikiumwa nibembeleze
Usinipepee nipulize
Wana wana wana wana
Pale tulipokutana
Mikono tukapeana
Macho yakatizamana
Wana wana wana wana
Pale tulipokutana
Namba kubadilishana
Nafsi kukubaliana oooh!
WATCH VIDEO
ABOUT THIS SONG
Release Year : 2020
Album : Zuchu Wana (Cover)
Copyright : (c) 2020
Added By : Huntyr Kelx
SEE ALSO
AUTHOR
GOLD BOY
Tanzania
Gold Boy is an artist from Tanzania best known for popular music covers. ...
YOU MAY ALSO LIKE