Narudisha Lyrics
Abudiwa Bwana, tukuka Bwana,
Heshimika Bwana, tukuka milele,
Wewe ni Mungu hakuna kama wewe Bwana,
Unayotenda hakuna mwingine awezaye tenda,
Unarudishia watu miaka yao, waliopoteza
Ulimrudishia Ayubu miaka yote aliopoteza,
Mali yake watoto wote bwana ulirudisha,
Tena maradufu,
Miaka yangu iliyoliwa na nzige,
Bwana ulirudisha nami najua nitarudishiwa,
Miaka yangu nitarudishiwa,
Iliyoliwa na nzige nitarudisha,
Eeeiee miaka yangu,
Iliyoliwa na nzige,
Narudisha! narudisha!
Miaka yangu iliyoliwa na nzige,
Narudisha kwa jina la Yesu
Miaka yangu, iliyoliwa na nzige,
Narudisha kwa jina la Yesu.
Nzige wamekula amani ya wengi,
Nzige wameharibu afya ya wengi mno,
Angalia imebaki mifupa mikavu,
Tazama imebakia mifupa mikavu,
Lakini kuna tumaini, Bwana atarudisha,
Amani itarudishwa, afya itarudishwa,
Biashara itarudishwa, furaha inarudishwa,
Waliopakwa tope, Bwana anasafisha,
Walioshushwa chini Bwana anainua,
Ata mti ukikatwa, utachipuka tena,
Waliopoteza maono yao jipe moyo,
Bwana anarudisha kwa jina la yesu
Narudisha, narudisha,
Miaka yangu, iliyoliwa na nzige,
Narudisha kwa jina la Yesu,
Miaka yangu iliyoliwa na nzige,
Narudisha kwa jina la Yesu.
WATCH VIDEO
ABOUT THIS SONG
Release Year : 2017
Album : Narudisha (Single)
Copyright : ©2017
Added By : Trendy Sushi
SEE ALSO
AUTHOR
GLORIA MULIRO
Kenya
Gloria Muliro is a Kenyan Gospel Musician who was born in Emuhaya, Western of Kenya to the late Davi ...
YOU MAY ALSO LIKE