Glory ft Gifted Lyrics
Nilikua kama DIRA.. sina kazi baada ya chombo kutia nanga
au kama TIBA.. sikuwa na mchongo baada ya mgonjwa kukata kamba
MSHUMAA uliozimwa baada ya machweo kutanda
SHUJAA aliyeminywa.. wenye vyeo waweze tamba
nilitupwa kama pingu ya mfungwa alityetoka jela
Au fimbo ya kipofu baada ya mpofu kuiona hela
au mkono wa mzazi baada ya mtoto kujua kutembea
Nilisuswa kama boya mbele ya wajuaji wa kuogelea
nilishiwdwa kila vita.. nilipigika kama mjinga
Sikuwahi kuamini, kuna siku na Mimi wataanita bingwa
Wenzangu ikaanza kuwalipa.. mbona kwangu miamala haisomi?
Nikaumiza kichwa ili mipango isigome
Wakiweka milima Mimi ninaigeuza vitonga
Hata nusu hatua ni hatua.. mdogo mdogo nikawa ninasonga
Japo ni kwa mwendo wa kinyonga
Mbegu ili kuchipua lazima ioze kwanza mjomba
Mtaani ninakuta wana wananisemasema siwezi
Ndani yangu ninasikia sauti inaniambia jamaa unaweza
Anguko lina herufi sita, MUAMKO linazo pia
Huzuni ina herufi sita.. FURAHA inazo pia
Utukufu ni wako baba..Sifa zote unastahili
Sio leo tu, hata jana.. umeonyesha unanipenda mimi
Niilijihisi kama.. koroboi lilozimwa mida ya machweo
Fukofuko lilotoswa kiwavi ageuke kipepeo
Maswali yaliyokwisha baada ya elimu kupatikana
Sikujua. mapito niliyopita ni kipimo cha uungwana
Niliachwa kama kiota,ndege alipojua kupaa
Mateso hayakua ajali,bali ni mzani wa ushujaa
Nilikua ninanuka.. haukuona kinyaa
Ulininyanyua nikanyanyuka.. sasa kila kona ninang’aa
Niliyoyapitia yalionyesha nguvu niliyonayo
Majaribu yakauibua ujasiri niliopewa na Mayo
Nikawa hodari.. nikaweza kuukabili utata
Ndoto niliyokua nayo imegeuka uhalisia sasa
Umefanya nijiamini pasina kuweka chembe ya uoga.. nimekubali
Nilihitaji nianguke, ili ninyanyuke nikiwa ngangari
Nisikate tamaa au kuhofia
KUJIKATAA ina herufi tisa.. KUJIAMINI inazo pia
Utukufu ni wako baba
Sifa zote unastahili
Sio leo tu, hata jana.. umeonyesha unanipenda mimi
WATCH VIDEO
ABOUT THIS SONG
Release Year : 2024
Album : (Single)
Added By : Farida
SEE ALSO
AUTHOR
FID Q
Tanzania
Fid Q, born Fareed Kubanda on the 13th of August 1982 in Mwanza, Tanzania, is a popular Bongo F ...
YOU MAY ALSO LIKE